Header Ads Widget

SHALOM AKUTANA NA MWENEZI CCM MKOA WA IRINGA

Mwandishi wa habari kutoka Mkoani Iringa Shalom Robert leo December 28.2024 amefika katika ofisi za makao makuu ya Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Iringa na kufanya mazungumzo na Mwenezi wa CCM Mkoa wa Iringa Ndg.Joseph Nzala Ryata.

Pamoja na mambo mengine Shalom amempongeza Ryata kwa kazi kubwa ya uenezi anayoifanya katika Mkoa huo katika kuhabarisha umma kuhusu kazi inayofanywa na serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan.

Aidha Shalom amesema wajibu wa chama ni kusimamia ilani ya uchaguzi ambayo kwa Mkoa wa Iringa inaendelea kutekelezwa kwa kishindo.

Ryata pia amempongeza mwanahabari huyo kwa kazi kubwa anayoifanya ya kuhabarisha umma kuhusu masuala mbali mbali huku akimpongeza kwa kuwa kiunganishi baina ya wananchi,serikali na chama kupitia taaluma yake.



 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI