Header Ads Widget

RAIS BASHAR AL -ASSAD APINDILIWA

 



-Rais Bashar al-Assad ameripotiwa kukimbilia kusikojulikana.

Na Matukio Daima media 

Baada ya Waasi kuudhibiti  Mji Mkuu wa Damascus alfajiri ya leo, Desemba 8, 2024, kumemlazimisha Rais wa nchi hiyo kutorokea kusikojulikana na kuiacha nchi mikononi mwa kundi hilo la waasi.

Vyanzo vya ndani na nje ya nchi hiyo, vinasema kitendo cha Rais Al Assad kukimbia kinamaliza  ukomo wa Utawala wa Miaka 53 wa Familia ya Assad.

Kiongozi wa Waasi wa Kundi la Hayat Tahrir al-Sham, Abu Mohammed al-Julani amesema Taasisi zote za Serikali zitabaki chini ya usimamizi wa Waziri Mkuu,  Mohamed Ghazi al-Jalali kwa kipindi hiki.

Kiongozi huyo wa kundi la waasi amesema baada ya kukamilisha mpango wa kumuondoa Assas madarakani watawaachia watu wa Syria kuchagua kiongozi wanayemtaka.

Wakati hali hiyo ikitokea maelfu ya wananchi katika mji wa Da wamejitokeza Damascus barabarani na kwenye viunga mbalimbali kusheherekea huku wakibandua mabango yenye picha za kiongozi huyo aliyekimbia.

Taarifa zaidi kutoka Iraq zinasema Taifa hilo limewapokea askari zaidi ya 2,000 wa serikali ya Assad ambao wametorokea katika nchi hiyo wakiwa na vifaa vya vita baada ya kukimbia mapambano nchini Syria.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI