Header Ads Widget

JOHN DUMELO AJITANGAZA MSHINDI WA UBUNGE

 


Mgombea ubunge kupitia Chama cha National Democratic Congress (NDC) John Dumelo amejitangaza mshindi wa eneo bunge la Ayawaso West Wuogon dhidi ya Lydia Alhassan katika uchaguzi mkuu wa 2024.


Dumelo ambaye ni muigizaji, mfanyabiashara, na mwanasiasa kutoka Ghana, ametikisa jukwaa la kisiasa na kuibua hoja juu ya uwezekano wa ushindi wa kihistoria kwa chama cha upinzani cha NDC kinacho ongozwa na Rais wa zamani, John Mahama ambaye naye anagombea.


Ikiwa itathibitishwa, ushindi huo utakuwa wa kwanza kwa NDC baada ya 24 miaka.


"Bado vituo 13 vya kupigia kura, naweza kusema kwa ujasiri tumeshinda kiti cha Ayawaso West Wuogon kwa kwa mara ya kwanza baada ya miaka 24," mwigizaji huyo aliyegeuka mwanasiasa aliandika kwenye ukurasa wake wa Facebook Jumapili, Desemba 8, 2024, akiashiria ushindi wake unaotarajiwa.


Tangazo hilo linafuatia mpambano mkali dhidi ya Lydia Alhassan, mbunge wa sasa kupitia chama tawala cha New Patriotic Party (NPP). Wengi waliamini kuwa Lydia Alhassan angeendelea kushikilia kiti chake kwa sababu eneo bunge hilo kihistoria limekuwa ngome ya NPP.


Hata hivyo, vijana na upigaji kura mbalimbali wa eneo bunge unaonekana vinginevyo.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI