Header Ads Widget

PWANI KUFANYA MAONYESHO YA UWEKEZAJI NA BIASHARA

 

MKOA wa Pwani umeandaa maonyesho ya wiki ya Uwekezaji na Biashara yatakayofanyika Wilayani Kibaha kuanzia Desemba 16 hadi 20 mwaka huu.

Hayo yamesemwa Mjini Kibaha na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake na kuwa maonyesho hayo yatawashirikisha washiriki 550. 

Kunenge amesema kuwa maonyesho hayo yatafunguliwa Desemba 17 na yatafanyika kwenye viwanja vya iliyokuwa stendi ya zamani ya Maili Moja Kibaha ambapo wahudhuriaji wa maonyesho hayo wanakadiriwa kuwa 25,000.

Aidha amesema kutafanyika kongamano Desemba 18 ambapo kutakuwa na wataalamu mbalimbali, wabobezi wa masuala ya biashara na mada mbalimbali na kupata taarifa zitakazoboresha biashara.

Ameongeza kuwa mkoa umejipanga vizuri hasa ikizingatiwa kuwa Mkoa una viwanda 1,553 na tangu Rais aingie madarakani viwanda vikubwa ni 78.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI