Header Ads Widget

ANDENGENYE AZINDUA BODI KUWASA, ATAHADHARISHA BEI YA MAJI

Na Fadhili Abdallah, Kigoma

MKUU wa mkoa Kigoma Thobias Andengenye ameiasa Mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira Kigoma Ujiji (KUWASA) kutochukulia  kuboreshwa kwa upatikanaji wa huduma za maji safi na salama katika manispaa ya Kigoma Ujiji kuwa kichocheo cha kuongeza bei ya maji ambayo itakuwa mzigo mkubwa kwa wananchi kuimudu.

Andengenye alisema hayo akizindua bodi ya tisa ya KUWASA baada ya kumaliza muda wake kwa wajumbe wa bodi ya nane ya Mamlaka hiyo kwa mujibu wa sheria na kwamba  anaipongeza bodi inayomaliza muda wake kwa kazi kubwa iliyofanya katika utekelezaji wa miradi ya maji katika manispaa ya Kigoma Ujiji na vitongoji vyake.

Mkuu huyo wa mkoa alisema kuwa badala ya Bodi mpya kuongeza gharama za huduma kwa wananchi itafute mbinu mpya ambayo itachagiza kupunguza huduma za uendeshaji na uzalishaji maji ili wananchi wapate nafuu ya gharama lakini kuendelea kupata huduma ya maji safi na salama wakati wote.

Pamoja na hilo Mkuu huyo wa mkoa alisema kuwa kukamilika kwa mradi mkubwa wa maji wa Amani Beach Mjini Kigoma kumechochea utekelezaji wa miradi mikubwa ya maendeleo mkoani humo sambamba na kutoa nafasi kwa watu mbalimbali kufanya shughuli nyingine za maendeleo badala ya kutumia muda mwingi  kutafuta maji.

Awali Mkurugenzi Mtendaji wa KUWASA,Poas Kilangi alisema kuwa kukamilika kwa mradi mkubwa wa maji kumewezesha uzalishaji kufikia lita milioni 42 kwa siku lakini kwa sasa wanazalisha  lita milioni 18 hadi 23 kwa siku kutokana na mahitaji huku upatikanaji wa maji ukifikia asilimia 92 kutoka asilimia 75 kabla ya kukamilika kwa mradi.

Pamoja na mafanikio hayo alisema kuwa mpango wa mamlaka ni kuongeza mtandao wa maji katika kata zilizopo nje ya manispaa ya Kigoma Ujiji na kwamba serikali imetoa kiasi cha shilingi Bilioni 2.9  kutekeleza mradi wa ujenzi wa tank la kupeleka maji maeneo hayo ambapo kukamilika kwa miradi hiyo kuitaifanya mamlaka kufikia asilimia 95 ya utoaji huduma kwa wananchi.

aidha Mkurugeni huyo amesema kuwa wanataka kuanzisha mchakato wa kuongeza bei ya maji kwani iliyopo imepitwa na wakati kutokana na kuongezeka kwa gharama za uzalishaji na uendeshaji

Akizungumza katika uzinduzi huo Mwenyekiti wa bodi ya tisa ya KUWASA, Kalist Zabuhakwa alisema kuwa moja ⁰nya malengo makubwa ambayo ataanza nayo na kuyasimamia ni kukamilisha lengo la utoaji huduma za maji kwa wananchi kufikia asilimia 95 mwaka 2025.

Sote tunajua maji ni bure lakini gharama inakuja kwa ajili ya utengenezaji wa miundo mbinu ambayo inawezesha huduma ya maji kufika kwa wananchi na huduma kuwa rahisi hivyo bei kubwa isiwe sababu ya wananchi kuchukia huduma za mamlaka hiyo.

 uzalishaji maj umefikia na mpango ni kuongeza mtandao maeneo ya nje ya manispaa ya Kigoma imetolewa kwa kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya miradi ya maji katika Mamlaka ya maji safi na maji taka Kigima Ujiji mkoani Kigoma .



 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI