Chama cha ACT-Wazalendo kupitia Ngome ya vijana kimesema kuwa wameambiwa na madaktari wanaomuuguza Mwenyekiti wa Ngome hiyo, Abdul Nondo aliyetekwa na watu wasiojulikana kuwa mwili wake umejaa kiwango kikubwa cha sumu.
Kupitia taarifa kwa umma iliyotolewa na Philibert Macheyeki Katibu wa uenezi wa ngome hiyo amesema kuwa madaktari wa Agha Khan hawajabaini sumu ya aina gani iliyomo kwenye mwili wa Nondo.
"Madaktari wamedai mwili wa Abdul Nondo unaonyesha kuwa na kiwango kikubwa cha Sumu ambayo mpaka sasa hawajajua kama zimetokana na athari za kupigwa na kuteswa au kama alipewa kitu chenye sumu na watekaji wake," ilisema Taarifa hiyo.
Hata hivyo madaktari hao walimfanyia upasuaji mdogo kwenye nyayo za Nondo kutokana na kuvunjikia vitu wakati alipokuwa akiteswa.
Taarifa hiyo inaeleza kuwa hali ya Nondo haijaimarika anaendelea na matibabu.
0 Comments