Header Ads Widget

MWENYEKITI WA KITONGOJI UPINZANI AFUNGUKA, AOMBA USHIRIKIANO NA CCM

 

Na Fadhili Abdallah,Kigoma

MWENYEKITI pekee wa kitongoji anayetokana na chama cha ADC, Bwana  Mtoro Bakari Mvunye ameomba watendaji wa serikali na Chama Cha Mapinduzi katika halmashauri ya wilaya Kigoma kumpa ushirikiano ili kuweza kutimiza dhamira yake ya kuwatumikia wananchi kwa mafanikio.

Mvunye ambaye ni mwenyekiti wa kitongoji cha Mwandiga Kaskazini kwenye mji mdogo wa Mwandiga Halmashauri ya wilaya Kigoma akiwa pia Mkurugenzi wa uchaguzi Taifa wa Chama cha  ADC alisema kuwa dhamira yake ni kuwatumikia wananchi katika kusaidia kutatua kero zao na kuwaletea maendeleo kulingana na mipango inayopangwa na serikali.

Akizungumza mbele ya Katibu wa siasa, uenezi na mafunzo CCM mkoa Kigoma, Deogratius Nsokolo aliyembetelea nyumbani kwake kumpongeza kwa ushindi huo Mwenyekiti huyo alisema kuwa kwa sasa serikali inaongozwa na Chama tawala CCM huku Diwani na Mbunge wote wakiwa CCM hivyo kushirikiana na viongozi hao kutamwezesha kutekeleza majukumu yake kwa mafanikio

Akizungumza na mwenyekiti huyo wa kitongoji nyumbani kwake alipomtembelea Katibu wa Siasa,uenezi na mafunzo  CCM mkoa Kigoma, Deogratius Nsokolo alimpongeza Mwenyekiti huyo pekee anayetokana na chama cha ADC kwa ushindi alioupata ambao unampa nafasi ya kuwatumikia wananchi.

Nsokolo alimuomba Mwenyekiti huyo kuwa baada ya kushinda kiti hicho cha kitongoji anapaswa kufanya kazi na vyama vyote ikiwemo CCM kwa kuunda baraza la ushauri la vyama mchanganyiko kwani Pamoja na ushindi huo wapo pia wanachama wa CCM ambao ni wananchi wake na wengine mmoja mmoja walimpigia kura wakiona anafaa kuwaongoza.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI