Na Fadhili Abdallah,Kigoma
Mwenyekiti wa CCM mkoa Kigoma Jamal Tamim ametoa salam za mwaka mpya kwa viongozi wa CCM, wanachama na wananchi wa mkoa Kigoma akiwataka watu wote mkoani humo kuachana na mambo mabaya na kutokubali kuchonganishwa na serikali yao.
Tamim alisema hayo mjini Kigoma akizungumza na waandishi wa habari ambapo katika salam zake hizo za kuuaga mwaka 2024 na kuukaribisha mwaka 2025 amepongeza kazi kubwa iliyofanywa na serikali ya awamu ya sita chini ya Raisi Samia Suluhu Hassan.
Katika salamu zake mwenyekiti huyo amewatakai heri na baraka viongozi wote wa serikali wawe na afya njema kwa mwaka 2025 huku akihimiza upendo, amani na mshikamano miongoni mwao na viongozi wao akionya Watanzania kujihadhari na watu wenye uchu wa madaraka.
Kwa upande wake Sheikh wa mkoa Kigoma, Hassan Iddi Kiburwa akitoa salama za mwaka mpya amewatakia afya njema viongozi wote wakiongozwa na Raisi Samia Suluhu Hassan ambaye amefanya kazi kubwa ya kuwatumia watanzania katika kuwaletea maendeleo.
Kiburwa alisema kuwa Tanzania itajengwa na watanzania wenyewe ambapo mwaka 2025 ambapo Tanzania itafanya uchaguzi Mkuu wa Raisi, Wabunge na madiwani ameomba Mwenyezi Mungu kujaalia uchaguzi huo wa amani na salama.
0 Comments