Header Ads Widget

CHATANDA: WALIOHUSIKA NA MAUAJI YA ALIYEKUWA KATIBU WA CCM KILOLO WACHUKULIWE HATUA KALI*


Mwenyekiti wa Umoja wa wanawake Tanzania UWT  Taifa *Ndg. Mary Pius Chatanda (MCC)* amevitaka vyombo vya ulinzi na usalama kufanya uchunguzi wa kina na kuwachukulia hatua kali za kisheria kwa watakaobainika kuhusika kwa mauaji ya aliyekuwa Katibu wa CCM Wilaya ya Kilolo *Christina Kibiki*.

Chatanda amesema kuwa, watu wote wanaohusika na vitendo vya mauaji au vitendo vinavyopoteza amani na utulivu wanatia doa juhudi kubwa za kuimarisha ulinzi, usalama, amani na utulivu zinazofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita.

Chatanda ameyasema hayo hii leo alipokuwa akizungumza na wananchi wa Kilolo katika mkutano wa hadhara uliofanyika viwanja vya Ilula vilivyopo wilayani humo.

*"Pamoja na kazi kubwa anayoifanya Rais wetu ya kuimarisha  utulivu na amani, lakini wapo watu ambao hawaipendi  amani iliyopo  ndani ya nchi yetu, watu wa namna hii walaaniwe; tunaiomba Serikali iendelee kufanya uchunguzi  ili kuwabaini  waliofanya mauaji hayo na mara watakapopatikana hatua stahiki za kisheria zichuchukuliwe dhidi yao kwa unyama na ukatili waliofanya"* alisema.

#uwt imara
#jeshi la dkt samia na dkt mwinyi
#kaziiendelee


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI