Header Ads Widget

MASUDI MAMBO AJITOSA KUGOMBEA UENYEKITI BAVICHA TAIFA


Viongozi wa baraza la wazee CHADEMA mkoa Kigoma wakimvisha Masudi nguo ya asili ya kabila la Waha MPUZU ikiwa ishara ya kumuunga mkono katika nia yake ya kugombea nafasi ya uenyekiti BAVICHA Taifa


Mwanachama wa CHADEMA mkoani Kigoma Masudi Mambo akitangaza azma ya kugombea nafasi ya Uenyekiti wa Taifa BAVICHA

Na Fadhili Abdallah,Kigoma

MWANACHAMA wa Chama Cha Demokrasia (CHADEMA) mkoani Kigoma Masudi Mambo ametangaza nia ya kugombea nafasi ya Uenyekiti wa Taifa wa Baraza la Vijana wa CHADEMA (BAVICHA) katika uchaguzi unaotarajia kufanyika hivi karibuni.


Mambo ametangaza nia na dhamira yake yake hiyo mbele ya wajumbe wa BAVICHA jimbo la Kigoma Mjini akisema kuwa nia anayo na uwezo wa kuongoza taasisi hiyo ya vijana anayo.

Mwanachama huyo ambaye amemaliza shahada ya kwanza ya Sayansi ya Siasa kutoka chou kikuu cha Dar es Salaam alisema kuwa amekusudia kutumia nafasi yake hiyo kuwatumikia vijana wenzake ili kusaidia kukabili changamoto mbalimbali zinazowakabili vijana kupitia kwenye nafasi hiyo ya Mwenyekiti wa BAVICHA.

Kufuatia kutangaza azma hiyo viongozi na wazee wa CHADEMA mkoa Kigoma wametangaza kumuunga mkono mtia nia huyo ambapo kuthibitisha dhamira yao wamemtangaza kuwa Mwami Rusimbi akiwa mwami kijana ili kuwaongoza vijana wenzake kuelekea mafanikio.

Mwenyekiti wa CHADEMA jimbo la Kigoma Mjini Omari Gindi akitangaza azimio la chama hicho mkoani Kigoma Kumuunga mkono Masudi Mambo katika nia yake ya kugombea nafasi ya uenyekiti BAVICHA Taifa

Mwenyekiti wa CHADEMA jimbo la Kigoma Mjini, Omari Gindi akizungumza baada ya mtia nia huyo kutangaza dhamira yake hiyo alisema kuwa Kigoma wamekubaliana kumuunga Masudi Mambo katika harakati zake za kuwania nafasi ya Mwenyekiti wa BAVICHA na kwamba watamsaidia kwa hali na mali kufanikisha dhamira hiyo kwani kwa sifa alizonazo wanaamini anastahili.

Kwa upande wake Mjumbe wa baraza la wazee CHADEMA mkoa Kigoma, Shaban Madede ambaye ni Katibu wa Mkoa Mstaafu wa CHADEMA alisema kuwa  Kigoma wamekubaliana kumuunga mkono Masudi Mambo kugombea nafasi kwani kwa sifa alizonazo zinatosha kumpa nafasi hiyo luwatumikia vijana wenzake.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI