Baada ya Mwenyekiti wa Ngome ya Vijana wa Chama cha ACTWazalendo, Abdul Nondo kupatikana maeneo ya Coco Beach, Chama hicho kimetoa tamko na kueleza kuwa kinasikitishwa na Jeshi la Polisi kutolichukulia suala la watu kutekwa Watu kwa umakini
Wakizungumza na waandishi wa Habari leo Desemba 2, 2024, Viongozi wa Ngome ya Vijana wamesema tukio zima la utekwaji wa Abdul Nondo halijachukuliwa kwa uzito na Jeshi ya Polisi, bali kilichofanyika ni kutoa matamko ya 'jumla jumla'
Abdul Nondo aliripotiwa kuchukuliwa na Watu Wasiojulikana alfajiri ya Desemba 1, 2024 katika Kituo cha Mabasi cha Magufuli wakati akishuka kwenye basi akitokea Kigoma baadaye kupatikana akiwa ametelekezwa Coco Beach akiwa na Majeraha
0 Comments