NA ZUHURA ZUKHERY, MATUKIO DAIMA IRINGA.
Wakazi wamanispaa ya Iringa wametakiwa kudumisha usafi katika mji huo na maeneo mengine ili kuiwezesha halmashauri ya manispaa ya Iringa kuendelea kushikanafasi ya kwanza kitaifa katika usafi huku Mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi ya CCM Fadhili Ngajilo (vunja bei) akitoa kiasi cha shilingi laki mbili kwaajili ya kununua vifaa vya usafi katika soko kuu la manispaa ya Iringa.
Akikabidhi fedha hizo Fadhili Ngajilo (vunja bei) baada ya kuhitimisha zoezi la kufanya usafi katika soko kuu la manispaa ya Iringa lililo ratibiwa na umoja wa vijana wa ccm UVCCM wilaya ya Iringa mjini Ngajilo alisema kuwa halmashauri ya manispaa ya Iringa itaendele kushika nafasi ya kwanza katika usafi kama wananchi wote wataendelea kushikamana katika kusafisha mazingira yanayowazunguka.
Ngajilo alisema kuwa kushika namba moja taifa sio jambo dogo kwani wananchi kwa kushirikiana na manispaa ya Iringa walikuwa tayari kushirikiana katika kuimarisha usafi wa mazingira hali iliyoifanya manispaa ya Iringa kuwa ya mfano huku baadhi ya halmashauri wakitaka kujua mbinu zilizotumika kuufanya mji wa Iringa kuwa msafi.
Alisema kuwa maeneo mengi ukipita katika halmashauri ya manispaa ya I ringa utakuta watu wa usafi wa kiendela na kazi zao huku kila kona kukiwa kumewekwa madebe ya kutupa taka hali inayowafanya wananchi kutotupa takataka hovyo barabarani kwa kuwa madebe hayo yapo kila kona.
Alisema wakazi wa halmashauri ya mji wa Iringa ni waelewa pale wanapoelimishwa hivyo haijatumika nguvu kubwa kuwataka kuweka mji kuwa msafi na hakuna mwananchi aliyewahi kukamatwa au kupigwa faini kwa sababu ya kutupa taka hovyo.
“halmashauri ya manispaa ya Iringa kushika nafasi ya kwanza kitaifa sio jambo dogo hata kidogo kuna kazi kubwa imefanywa na meya wetu wa manispaa ya Iringa Ibrahimu Mwangwada na wafanyakazi wa manispaa ya Iringa na wananchi kwa ujumla ukitembelea masoko yite ni masafi ukienda stendi za mabasi kote kusafi lakini ukifika katika hospitali zetu zote ni safi barabarani huko ndio usiseme ni kusafi sana ni seme tu hii kazi wanayoifanya ya usafi ipo hata katika ilani ya chama cha mapinduzi hivyo niwahamasishe vijana hawa wa ccm na jumuiya zote za chama kuendelea kuunga mkono juhudi za utunzaji mazingira”a alisema Ngajiro.
Aidha Ngajilo alisema kuwa halmashauri ya manispaa ya Iringa ni lango la kuingia katika vivutio vya utalii hivyo wanachi wa manispaa ya Iringa ikiendelea kudumisha usafi watalii wataongezeka na pato la taifa litaongezeka kupitia utalii.
Alisema kuwa watalii wanapenda kutembea maeneo ambayo ni masafi na yanavutia kuangalia na Iringa ni sehemu ya utalii hivyo hapatakiwi kuwa na mazingira machafu ili tuendelee kupokea wageni wakutosha watakaotembelea vivutio vyetu.
Alisema kuwa mji wa Iringa una hali ya hewa nzuri uklinganisha na maeneo mengine hivyo usafi ukiendelea kudumishwa idadi ya watalii wataongezeka kwani wengi wao hupenda kutembelea maeneo yenye hali ya hewa ya ubaridi.
“ ndugu zangu Iringa tuna vitu vingi sana vya kitalii lakini ili uvifikie vituo vya utalii lazima upite halmashauri ya manispaa ya Iringa, ukitaka kwenda makumbusho ya Mtwa Mkwawa , Isimila hifadhi ya taifa Ruaha na maeneo mengine mengi ni lazima ufike halmashauri ya manispaa ya Iringa hivyo naipongeza sana halmashauri ya manispaa ya iringa na wananchi wote kwa ujumla niseme tu Iringa uchafu sasa basi” alisema Ngajilo
Kwa upande wake mwenyekiti wa masoko manispaa ya Iringa Raphael Ngullo licha ya kuwashukuru UVCCM kwa kufanya usafi katika siko hilo alisema kuwa soko kuu la manispaa ya Iringa linakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo changamoto mfumo wa fedha za ununuaji wa umeme katika soko hilo.
Alisema kuwa fedha kutoka manispaa ya Iringa kwa ajili ya manunuzi ya umeme yamekuwa ni shida hivyo amekiomba chama cha mapinduzi kuingilia kati ili manispaa waruhusu uongozi wa masoko kutoa fedha za ushuru wa soko katika matumizi muhimu.
Aidha amemuomba mwaenyekiti wa jumuiya ya wazazi wa CCM mkoa wa Iringa Fadhili Ngajilo meya wamanispaa ya Iringa na wote wenye mamlaka kuhamasisha halmashauri ya manispaa ya Iringa kutoa fedha millioni 17 zilizotoka mwezi july mwaka huu kwaajili ya ukarabati wa masoko zitolewe ili kurabati uanze kufanyikaa.
“ ndugu mwenyekiti wa wazazi Ngajilo, mwenyekiti Uvccm na meya nyie ni wajumbe wa kamati katika CCM tunaomba mtufuatilie fedha million 17 za ukarabati wa masoko zilizotoka tangu mwezi july tunaomba muwaambie fedha za ukarabati wa miradi zikifika zitolewe haraka ili miradi husika ianze kufanyiwa kazi, tunasoko lipo kitanzini lile soko lilikosewa kujengwa paa zake zipo chini hivyo hakuna mfanya biashara anayefanyia kazi katika soko hilo walete hela tukarabati soko lianze kufanya kazi” alisema Ngullo
Aidha aliwataka vijana kuendeleza kutunza mazingira kwa kushiriki kampeni ya upandaji miti inayojulikana kama mti wa mama jambo ambalo watakuwa wamemuenzi Rais wajamuhuri ya muungano wa tanzania dkt. Samia Suluhu Hassan.
Naye katibu wa elimu malezi na mazingira wa jumuiya ya wazazi wa CCM wilaya ya Iringa mjini Nguvu Chengula alisema kuwa jambo la usafi linapaswa kuzingatiwa na kila mmoja bila kujali itikadi za kisiasa wala dini kwani usafi umetajwa kila sehemu katika mzunguko wa maisha.
Alisema kuwa uongozi wa soko kuu la manispaa ya iringa unapaswa kupongezwa na kila mmoja kwani soko hilo limekuwa safi katika kipindi chote cha mwaka.
Aidha Nguvu aliwapongeza watumishi wa halmashauri ya manispaa ya Iringa akiwemo meya wa manispaa hiyo kwa kuendelea kusimamia vyema usafi wa mazingira katika manispaa ya Iringa.
Mwenyekiti wa jumuiya ya umoja wa vijana wa CCM Isack Kikoti aliwashukuru club ya mazoezi ya Iringa kwa kushikiana katika usafi wa soko hilo huku mwenyekiti wa club ya mazoezi Iringa Samwel Komba akiwahamasisha wananchi kufanya mazoezi ili kukabiliana na magonjwa yatokanayo mwili kutokuwa na mazoezi.
Komba alisema kuwa mazoezi sio lazima kukimbia au kucheza mpira bali hata kufanya usafi wa mazingira nayo ni mazoezi tosha tofauti na mtu aliyekaa bila kufanya kazi yoyote.
0 Comments