Header Ads Widget

BALOZI DKT.CHANA AIPONGEZA NCAA KWA UKUSANYAJI WA MAPATO

 


Na,Jusline Marco:Arusha


Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Dkt. Pindi Chana ameipongeza Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro NCAA kwa kuonesha kasi katika ukusanyaji wa mapato ya shilingi bilioni 138.6 kwa kipindi cha miezi 4 ambapo ameitaka mamlaka hiyo kuongeza kasi zaidi ya ukusanyaji waapato hayo.


Dkt.Chana ameyasema hayo katika hafla ya uvalishaji cheo na uapisho wa Kamishna wa Uhifadhi NCAA Dkt.Elirehema Joshua Dorie ambapo amesema kati ya mwezi Julai hadi Novemba mwaka huu Mamlaka hiyo imekusanya kiasi hicho cha fedha huku zaidi ya watalii laki 5 wa nje na watalii zaidi ya laki 2 wakitembelea eneo la hifadhi katika kipindi hicho.


Aidha amepongeza uwepo wa matumizi ya teknolojia ya habari na mawasiliano Tehama katika eneo la hifadhi kutokana na uimarishwaji wa mifumo hiyo hatua inayoenda sambamba na mipango ya serikali ya kuimarisha utendaji kupitia teknolojia.


Ameongeza kwa kuitaka Mamlaka hiyo kuendelea kuimarisha miundombinu ikiwemo barabara namadaraja huku akiotaka kuifanya kuwa miongoni mwa agenda zao katika utendajikazi.


Dkt.Chana ameielekeza NCAA kupanua wigo wa watalii ma Utalii kwa kutenga mipango bora itakayowawezesha kuvutia vivutio ikiwepo Oldupai Gorge ,mapango ya amboni ,kimondo cha mbozi na maeneo mengine ya utalii ili kuvutia watalii zaidi kwenye vivutio vya mambo kale.


Mwenyekiti bodi ya Wakurugenzi NCAA Jenerali Mstaafu Venance Mabeyo katika hafla hiyo amesema bodi ya wakurugenzi wa NCAA inaamini uwezo na uzoefu wa Kamishna Dkt. Dorie alionao katika uongozi ambao utasaidia mamlaka kufikia malengo yake.


Amesema kwa niaba ya bodi hiyo wanategemea uongozi,weledi,uzalendo ,uvumilivu ,maono alionao katika kusimamia ihifadhi endelevu na kuendeleza utalii ambapo bodi hiyo imeahidi kushirikiana kuhakikisha kila jambo linatekelezwa kwa ufanisi.


Kamishna wa Uhifadhi NCAA Dkt.Elirehema Joshua Dorie amesema ili kuhakikisha Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro inabaki kuwa kivutio kinachoongoza duniani,kwa kuahirikiana na wadau wa ndani na nje ya nchi watahakikisha Utalii unachangia zaidi katika pato la taifa na maendeleo ya jamii.


Amesema dhamira yake kuu ni kusimamia uhifadhi endelevu kwa kuhakikisha rasilimali za kiasili na kihistoria zinalindwa na kisimamia matumizi endelevu ya teknolojia na uahirikishwaji wa jamii katika kutunza mazingira ambapo pia atahakikisha anakuza utalii wa kimkakati ambao ndiyo lango la fursa katika nchi na kuimarisha miundombinu,huduma na ubora wa vivutio vilivyomo ndani ya hifadhi ya ngorongoro.


Vilevile amesema atahakikisha anabuni na kuendeleza mipango yenye tija inahoheshimu maisha na kuhifadhi mazingira ya eneo la Hifadhi sambamba na kuboresha maslahi ya wafanyakazi ambao ndiyo nguzo muhimu ya Taasisi ua NCAA kwa kuwapatia motisha,mafunzo ya mara kwa mara ili kuimarisha hari yao ya kazi.




Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI