Header Ads Widget

WATAALAM WA MIONZI NCHINI WAPATIWA MAFUNZO YA MATUMIZI SAHIHI YA MIONZIYA ATOMU KWA WAGONJWA.

Na,Jusline Marco;Arusha

Tume ya Nguvu ya Atomu Tanzania imetoa mafunzo ya kitaifa ya kinga ya mionzi kwa wataalam wapatao 60 wenye sifa na ambao wanatumia vifaa vya uchunguzi Katika hospitali zenye vifaa vya kitaalam nchini.

Mkurugenzi wa Udhibiti na Usimamizi wa Mionzi kutoka Tume ya Nguvu za Atomu Tanzania TAEC Dkt.Justine Ngaile ameyasema hayo katika ufunguzi wa semina hiyo ya siku 5 kwa wataalum hao kutoka tanzania bara lengo likiwa ni kuwajengea uwezo wa matumizi salama ya mionzi jinsi ya kujikinga.

Dkt.Ngaile amesema mafunzo hayo ni muhimu kwa wataalam hao kutokana na huduma ya mionzi wanayoitoa katika kutumia vifaa vya uchunguzi ikiwemo X-ray,MRI na CT scan ambapo amewataka wataalam hao kuchukuwa kinga maalum ya kujikinga dhidi ya mionzi hiyo ili wasiweze kupata madhara wakati wa matumizi.

Ameongeza kwa kusema lengo kuu ni kutoa elimu juu ya matumizi sahihi ya vifaa vinayotoa mionzi na namna ya kuweza kujikinga na kumkinga mgonjwa anayepatiwa huduma ya mionzi ikiwa ni sambamba na kuwakinga watu wanaliokaribu na jengo lenye vifaa hivyo vya mionzi.

Ameleza kuwa Tume ya Nguzu za Atomu kama mdhibiti mkuu wa mionzi hiyo ina ruhusu wataalam wenye sifa kutoa huduma ya mionzi kwa wagonjwa ambapo amesema Tume hiyo intachukuwa jukumj ya kumzuia mtu ambaye atabainika kuendesha mitambo ya mionzi bila utaalam wowote ikiwa ni sambamba na kucjukuliwa hatua za kisheria.

Naye mmoja wa Wataalamu walioshiriki semina ya Mafunzo hayo Cathetine Malika mbaye ni Mkufunzi wa kutoka Chuo cha Afya Muhimbili amesema mafunzo hayo yatawasaidia wataalam hao kutoa mionzi inayokubalika kwa mgonjwa kulingana na kipimo sahihi ili kuweza kumlinda mgonjwa dhidi ya mionzi ya ziada ambayo ni hatari.


Amebainisha kuwa ni jukumu la wataalam kuhakikisha anajilinda,analinda mgonjwa na kulinda jamii inayowazunguka dhidi ya madhara ya mionzi.



 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI