Header Ads Widget

ACT WAZALENDO WALIA NA CHANGAMOTO ZINAZOWAKABILI WANAWAKE ZANZIBAR

 


NA MWANDISHI WETU,ZANZIBAR –MATUKIO DAIMA 


CHAMA cha ACT Wazalendo kimesema kwamba Wanawake Visiwani Zanzibar bado wanakabiliwa na changamoto nyingi zikiwemo Ubaguzi, Udhalilishaji, Unyanyasaji na ukakatili wa kijinsia pamoja na ukosefu wa fursa sawa katika maeneo mbalimbali ya maisha yao.


Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari Msemaji wa Sekta ya Maendeleo ya Wanawake, Watoto na Makundi Maalum Zanzibar, Halima Ibrahim Mohammed amesema ongezeko la matukio ya ukatili, unyanyasaji na udhalilishaji wa kijinsia hayaoneshi hadhi na heshima ya Zanzibar kwani matendo hayo yapo kinyume na mila na tamaduni 


"Matukio ya udhalilishaji, ukatili na unyanyasaji kwa wanawake na watoto hayaonyeshi heshima ya Zanzibar kwani matukio hayo ni kinyume na mila, utamaduni na silka za Kizanzibari," amesema Halima 


Amesema, Hali hiyo ya ongezeko la matukio ya ukatili inasikitisha na inahitaji kudhibitiwa na wadau wote wakiwemo serikali, taasisi za jamii, dini, wazee kuacha muhali na kukubali kutoa ushahidi pia walimu na watoto kupewa elimu ya kujilinda na kujikinga dhidi ya watu waovu.


Sambamba na hilo, amesema wanawake wengi kisiwani hapa wanakumbana na changamoto ya ukosefu wa fursa za ajira jambo ambalo linasababisha kutegemea zaidi shughuli za kilimo, biashara ndogo ndogo na kazi za majumbani ambazo hazina malipo mazuri na kuwa wategemezi kwa waume na familia zao.


Pia, amesema licha ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kujenga hospitali za wilaya bado kuna changamoto katika huduma za afya ya uzazi, wanawake wengi wanakutana na changamoto za upatikanaji wa huduma bora za afya za uzazi ikiwemo huduma za kujifungua na upasuaji wa dharura.


"Upungufu wa wataalamu na vifaa katika hospitali nyingi, hii inasababisha wanawake kuwa katika hatari ya vifo wakati wa kujifungua, tatizo hili linaendelea kuwa kubwa zaidi baada ya hospitali ya Mnazimmoja kuhamisha huduma za uzazi katika hospitali ya Lumumba, ni wazi kwamba Hospitali hiyo imezidiwa na idadi ya watu wanaotaka huduma hii ya uzazi," amesema Halima 



kutokana na mambo hayo Msemaji huyo ameitaka serikali kuweka utaratibu maalum wa kina mama kuhudumiwa bila usumbufu wanapokwenda kujifungua katika hospitali ambazo zimehamishiwa huduma za kujifungua.


Pia, kufanya uchunguzi kampuni zinazosimamia ujenzi wa miundombinu na kuchukua hatua stahiki kwa wahusika na aliyehusika kusimamia makubaliano ya kuchukua fedha kama fidia ya udhalilishaji huo.


Vilevile serikali ihakikishe inasimamia sheria ya ukatili na unyanyasaji (gender based violence) ili kuondosha matukio ya udhalilishaji na ukatili wa kijinsia.


Pia, chama hicho kimewataka wananchi wanapoona kuna uvizishwaji wa kuendesha mashauri hayo wasisite kutoa taarifa kwa chama hicho na watatoa msaada wa kiushauri na kisheria ili haki isimame dhidi yao

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI