Header Ads Widget

POLISI WATOA TAARIFA YA HOFU YA KUTEKWA KWA ABDUL NONDO NA WATU WASIOJULIKANA.. ...

Mwenyekiti wa Ngome ya Vijana ya ACT Wazalendo Ndugu Abdul Nondo ametekwa asubuhi hii na watu wasiojulikana akitokea Mkoani Kigoma alikokuwa sehemu ya viongozi wa Kitaifa walioongoza kampeni kwenye Mikoa ya Magharibi mwa Tanzania.

Mashuhuda wa tukio wanasema kuwa kulikuwa na purukushani katika utekaji wa Nondo iliyosababisha begi lake ndogo kudondoka. Katibu Mwenezi Mkoa wa Dar es salaam Ndugu Monalisa Ndala na Afisa wa Harakati na Matukio Taifa Wiston Mogha waliofika mapema kituoni hapo walitambua haraka kuwa aliyetekwa ni Nondo kwa sababu walizitambua nguo zake kwenye begi lililodondoka na note book yake.

Chama kinaendelea kufuatilia taarifa zaidi kuhusu tukio hili na kitatoa taarifa zaidi kwa umma.

Katika hatua ya sasa tunamtaka Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Wambura kufuatilia mara moja na kuhakikisha Ndugu Abdul Nondo anaachiwa huru mara moja.  Anandika Ado Shaibu Katibu mkuu WA ACT wazalendo

Imetolewa na Mbarala Maharagande, Naibu Katibu wa Haki za Binadamu na Vyombo vya Uwakilishi wa Wananchi,

ACT Wazalendo.

1 Desemba 2024.

Simu: 0715 062 577

Kutokana na taarifa hii Matukio Daima media tumemtafuta kwa njia ya simu msemaji wa Jeshi la Polisi Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi SACP David Misime simu yake haijapokelewa na bado jitihada za kumtafuta zinaendelea .


TAZAMA VIDEO YA ZITTO KABWE BOFYA LINK HII

TWINITY MISSION SECONDARI SCHOOL YATANGAZA OFA KWA WAZAZI

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI