WASIMAMIZI wa Kemikali na Wamiliki wa viwanda wametakiwa kujiepusha na matumizi yasiyo salama ya Kemikali Ili kuepuka madhara yanayoweza kujitokeza kiafya na kimazingira kwa binadamu, wanyama, mimea na viumbe wengine.
Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za udhibiti kutoka Mamlaka ya maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, GCLA, Bw Mussa Kuzumila alisema hayo kwenye makao makuu ya Mamlaka hiyo Jijini Dodoma alipokutana na wasimamizi wa Kemikali na Wamiliki wa viwanda kutoka mikoa ya Dodoma, Morogoro , Tabora, Singida, Iringa na Ruvuma.
Akasema licha ya Kemikali licha ya Kemikali kuwa na umuhimu mkubwa kwenye masuala ya ki uchumi na kijamii, ina hatari kubwa iwapo matumizi sahihi na salama hayatazingatiwa
Akasema Mamlaka hiyo itaendelea kutekeleza matakwa ya Sheria ya Usimamizi na Udhibiti wa kemikali za Viwandani na Majumbani namba 3 ya Mwaka 2003 inayowataka kutoa elimu kwa makundi mbalimbali ya wadau wanaojishughulisha na kemikali pamoja na jamii Ili kuhakikisha matumizi sahihi na salama ya kemikali yanazingatiwa.
"Nia ya Serikali ni kuhakikisha malengo ya maendeleo endelevu kwa watu wote yanakuwepo ifikapo mwaka 2030, ndio maana tunazidi kuwaelimisha wadau wakati wote"Alisema Kaimu Mkurugenzi huyo.
Meneja wa Mamlaka ya Mkemia mkuu wa Serikali Kanda ya Kati Bw Gerald Meliyo Mollel, alisema Mamlaka hiyo itaendelea kuhakikisha matumizi ya kemikali yanakuwa salama wakati wote ili kuepusha madhara yanayoweza kujitokeza kwa afya za binadamu na mazingira kwa kufanya mafunzo kwa wadau.
"Tunajua bila elimu mambo hayawezi kwenda vizuri, lakini wanapokuwa na uelewa juu ya madhara ya kemikali na Kemikali ipi itumike kwa mazingira gani itasaidia sana,Kuna vitu muhimu pia wanapaswa kuwa navyo katika matumizi ya Kemikali ikiwemo vyeti maalum kutoka ofisi yetu na itawasaidia kutumia kemikali kwa usahihi"Alisema Mollel.
Akasema kuna Kemikali mbalimbali ambazo zina madhara makubwa zikiweno zinazotumika kwenye uchimbaji wa madini na ndio maana huwa zinahitaji usimamizi mzuri Ili kuepuka madhara.
Baadhi ya wasimamizi wa Kemikali na wamiliki viwanda akiwemo Katibu wa Vijana kutoka Chama cha wachimba madini wadogo Tanzania FEMATA,Samson Kadoke, mkemia Christina Haule kutoka Mamlaka ya Maji safi na usafi wa Mazingira Ruvuma na Levocatus Makongoloto wa Kampuni ya LEVOS, Levocatus Makologoto wakashukuru Serikali kupitia Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali kwa kuwapatia elimu hiyo ambayo itawasaidia wao na wengine katika shughuli zao za kila siku.
Kadoke akasema kundi kubwa la waathirika wa Kemikali ni vijana ambao wengi wamekuwa wanajishughulisha na uchenjuaji wa madini, eneo ambalo Kemikali hutumika kwa wingi, kutokana na kutochukuantahadhari na akwasihi watu wote wanaofanya shughuli hizo kuwa makini na kuzungatia matumizi salama kwasababu wanategemewa na familia zao na Taifa kwa ujumla.
"Sasa tutafahamu zaidi namna ya kujikinga na madhara yatakayotokana na kemikali"Alisema Levocatus.
0 Comments