Na Hamida Ramadhan,Matukio Daima app DODOMA
SEKTA ya matengenezo ya magari inakaribia kushuhudia mapinduzi makubwa baada ya kampuni ya THE WHEEL kuzindua teknolojia mpya ya kisasa inayolenga kuboresha utendaji wa mafundi na kuongeza ufanisi wa kazi zao.
Teknolojia hiyo, inayotumia akili bandia (AI) na mifumo ya uchambuzi wa data, inatarajiwa kubadilisha jinsi matatizo ya magari yanavyogunduliwa na kutatuliwa, hivyo kuokoa muda na kuongeza usalama kazini.
Akizungumza katika hafla ya uzinduzi,
imefungua kituo Cha utoaji huduma za urekebishaji wa haraka na utunzaji wa magari jijini Dodoma msemaji kutoka kampuni ya THE WHEEL amesema wamefurahi kupanua huduma hadi Dodoma ambapo lengo ni kuboresha uzoefu wa Uendeshaji Kwa wateja wao huku kituo hicho Ikiwa ni kituo cha saba Cha kutoa huduma nchini Tanzania.
Chris Mendoza, ameeleza kuwa teknolojia hii itawapa mafundi uwezo wa kugundua hitilafu kwa haraka zaidi, kupunguza muda wa matengenezo, na kuhakikisha magari yanarejeshwa kwa wateja katika hali bora zaidi.
Mendoza amesisitiza kuwa mafundi watahitaji mafunzo maalum ili kuendana na mabadiliko haya ya kiteknolojia, huku kampuni hiyo ikiahidi kushirikiana na vyuo vya ufundi ili kufanikisha lengo hilo.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa kampuni hiyo ya Amin Lakhani, alisema kuwa kufungua kituo Dodoma ni hatua muhimu kwa kampuni yao, hasa ikizingatiwa nafasi ya mji huo kama makao makuu ya nchi.
Lakhani ameeleza kuwa lengo ni kuwapa wateja huduma bora na salama zinazoboresha uzoefu wa uendeshaji wa magari.
Alitoa wito kwa wawekezaji wengine kuangazia fursa zilizopo Dodoma, akisema kuwa uwepo wa huduma za kisasa kama hizi utaimarisha uchumi wa mji na taifa kwa ujumla.
Aidha, alibainisha kuwa kituo hicho kitachangia kutoa ajira kwa vijana na kuboresha miundombinu ya usafiri katika eneo hilo.
TANGAZO LA NAFASI ZA MASOMO TWINITY MISSION SECONDARI SCHOOL MAFINGA IRINGA
0 Comments