Na Hadija Omary
Lindi....Jumla ya wenyeviti na wajumbe wa Serikali za mitaa na vitongoji 1953 wa Halmashauri ya Manispaa ya Lindi Mkoani Lindi wamekula kiapo cha uaminifu na uadilifu Katika majukumu Yao mapya
Zoezi Hilo limeongozwa na Hakimu Mkazi Mahaka ya Mwanzo Illuminata Lutakana mara baada ya viongozi hao kushinda uchaguzi uliofanyika Novemva 27 mwaka huu.
Mwanziva amesema viongozi hao ndio wanakutana na wananchi na kugundua changamoto zao hivyo wanapaswa kushughulika na mambo ya wananchi waliokuchagua bila kujali itikadi za vyama na dini zao.
Naye Msimamizi wa Uchaguzi Halmashauri ya Manispaa ya Lindi Juma Mnwele amewapongeza viongozi hao kuaminiwa na kuchaguliwa na kuwataka kufanya kazi kwa kuzingatia sheria, hasa kuepuka kuingilia majukumu ya kisheria ya vyombo vingine ikiwemo uuzaji wa viwanja.
Mwishoo
0 Comments