NA. HADIJA OMARY ,MATUKIO DAIMA APP, LINDI.
WAZIRI wa viwanda na Biashara Dtk. Selemani Jaffo amezitaka Halmashauri zote Nchini kupitia mapato ya ndani katika mikopo ya asilimia 10 kuwawezesha Vijana na Wanawake kutengeneza viwanda vinavyoakisi maeneo yao
Waziri Dkt. Jaffo ameyasema hayo Novemba 2, 2024 mara baada ya kuzindua Gulio la kwanza la biadhaa za ushonaji, Usindikaji Mkoani Lindi uliofanyika huko Katika viwanja vya Maonyesho nane nane Ngongo Manispaa ya Lindi.
Uzinduzi huo ulioenda sambamba na uzinduzi wa mfumo wa uuzaji wa bidhaa Mtandaoni uliopewa jina ya Lindi katika Uchumi wa Viwanda -E Soko (LIKUVI ) ambao utahusisha utangazaji na uuzaji wa bidhaa mtandaoni.
Amesema kuwa Halmashauri wanatakiwa kuendelea kutoa mikopo ya asilimia kumi ili kuwawezesha wajasiriamali wenye viwanda vidogo kufikia malengo yao.
"Niwatake viongozi wa Halmashauri zote,kuhakikisha wanatoa mikopo ya asilimia kumi kwa wajasiriamali hasa kwa wanawake na vijana ili kuwawezesha kuanzisha viwanda vidogo vidogo " .Dkt Jafo.
Hata hivyo Waziri Dokta Jaffo ameonyesha kuridhishwa na mfumo huo wa uuzaji wa Bidhaa mtandaoni ambapo Amesema mfumo huo utawawezesha wajasiliamali kuuza Bidhaa zao kwa urahisi kupitia mtandao
"Nimefurahia sana mfumo wa uuzaji wa bidhaa mtandaoni E- Sdoko, biashara za hapa nyingi zitakwenda kimtandao na wafanyabiashara wataweza kuuza zaidi . Ninyi mmekuwa Mkoa wa kwanza wa mfano kwa jambo ili , wengine wote watakuwa wanaiga kutoka mkoa wa Lindi. " Mhe. Dkt Jafo
Awali Mkuu wa Mkoa wa Lindi Bi. Zainab Telack alimueleza Waziri Dkt.Jafo namna mkoa wa huo ulivyojikita katika uzalishaji wa mwani na zao ufuta hivyo uwepo wa viwanda wa kuchakata na kusindika mazao hayo ni muhimu sana kwa Mkoa wa Lindi.
Mkuu wa divisheni ya viwanda biashara na uwekezaji mkoa wa lindi dokta bora haule amesema mkoa umejipanga kufanya gulio la namna hiyo mara mbili kwa mwezi ili kuwawezesha wajasiliamali kuuza na kutangaza bidhaa zao huku baadhi ya wafanyabiashara wakieleza matatizo wanayoyapata kwa kukosa viwanda vya usindikaji.
0 Comments