NA. ANDREW CHALE, MATUKIO DAIMA APP, DAR ES SALAAM.
WAWEKEZAJI Wafanyabiashara kutoka Jimbo la Bavaria nchini Ujerumani, wamevutiwa na fursa zilizopo Nchini hali inayofanya waendelee kuja Tanzania kufungua Masoko mapya.
Hayo yameelezwa na Naibu Waziri wa masuala ya uchumi wa Jimboa la Bavaria Nchini Ujerumani, Tobias Gotthardtd wakati ujumbe wa wafanyabiashara kutoka kampuni 35 katika Jimbo la Bavaria kukutana kwenye makazi ya Balozi wa Ujerumani, Dar es Salaam.
Amesema jimbo hilo lipo tayari kushirikiana na Tanzania kwa manufaa ya pande zote mbili hasa katika maeneo ya biashara, kilimo na sekta ya maji.
Mhe Tobias amebainisha kuwa, Ujumbe alioambatana nao umependezwa na fursa za kiuchumi zilizopo Nchini Tanzania hivyo wamepata kunadi biashara zao lakini pia wakiangalia namna bora za mashirikiano zaidi.
Kwa upande wake Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani, Hassani Mwamweta amesema Ujerumani ni mdau muhimu wa sekta ya teknolojia na uwekezaji wa kibiashara hapa nchini, na kwamba ataendelea kuibua fursa mbalimbali za ushirikiano.
Wawekezaji hao walipata fursa ya kufanya mazungumzo na kubadilishana mawazo na Wafanyabiashara wenzao wa Tanzania katika maongezi ya ana kwa ana.
Ujumbe huo wa Bavaria uliwasili Dar es Salaam kuanzia Oktoba 30 hadi Novemba 2, 2024. Ambapo Ujumbe huo umejumuisha viongozi kutoka nyanja za teknolojia ya mazingira, kilimo na chakula. viwanda, pamoja na wawakilishi kutoka wasomi na siasa.
Ziara hiyo imelenga kuimarisha uhusiano wa sasa na kuanzisha ushirikiano mpya kati ya Bavaria na Tanzania.
0 Comments