Header Ads Widget

UJENZI CHUO KIKUU MUHAS KAMPASI YA KIGOMA WAANZA


Makamu Mkuu wa chuo kikuu cha afya na sayansi shirikishi  Muhimbili (MHAS) Profesa Appolinary Kamuhabwa (kulia)  na Mkurugenzi  wa Kampuni ya China JIANGXI INTERNATIONAL AND TECHNICAL CO.LTD ya China Peng Chao wakionyesha mikataba waliyosaini kwa ajili ya ujenzi wa chuo cha MUHAS kampas ya Kigoma



Na Fadhili Abdallah,Kigoma


Chuo kikuu cha afya na sayansi shirikishi Muhimbili (MUHAS) kimetiliana saini na kampuni ya ujenzi ya CHINA JIANGXI INTERNATIONAL AND TWCHNICAL CO.LTD ya China kwa ajili ya ujenzi wa chuo kikuu cha MUHAS Kampasi ya Kigoma.



Utiaji saini huo umefanyika mkoani Kigoma katika eneo kitakapojengwa chuo hicho Eneo la KISEZ Ujiji mkoani Kigoma ambapo Makamu Mkuu wa Chuo MUHAS, Profesa Appolinary Kamuhambwa aliwakilisha chuo hicho huku Peng Chao akiwakilisha kampuni ya ujenzi ya CHINA JUANGXI INTERNATIONAL iliyoshinda tenda ya ujenzi wa chuo hicho.



Utiaji saini huo ulishuhudiwa na Mkuu wa mkoa Kigoma, Thobias Andengenye viongozi mbalimbali wa mkoa Kigoma, viongozi na watendaji wa MUHAS na wananchi wa mkoa Kigoma.



Akitoa maelezo kuhusu ujenzi wa chuo hicho Mratibu wa mradi wa Elimu ya juu kwa mageuzi ya uchumi (HEET).Profesa Erasto Mbugi alisema kuwa kiasi cha shilingi Bilioni 26 zitatumika kwa ajili ya ujenzi wa chuo hicho Kampasi ya Kigoma na ujenzi wake unapaswa kukamilika Mwezi Juni mwaka 2026.



Kwa upande wake Makamu Mkuu wa chuo Kikuu MUHAS, Profesa Appolinary Kamuhabwa  Akizungumza kabla ya kumkaribisha Mkuu wa mkoa alisema kuwa wanafunzi 5900 wanatarajia kudahiliwa na chuo hicho na kwamba ujenzi wa kampasi hiyo ni mradi wa kimkakati  wa serikali katika kupanua elimu ya juu katika sekta ya afya nchini.


Profesa Kamuhabwa alisema kuwa ujenzi wa kampasi hiyo ya Kigoma unatoa fursa kubwa katika kutoa mafunzo na kufanya tafiti hasa eneo lililopo imepakana na nchi za ukanda wa maziwa makuu hivyo kufanya kuwa na fursa  kubwa ya kufanya tafiti za magonjwa.



Mkuu wa mkoa Kigoma Thobias Andengenye akizungumza katika hafla ya utiaji saini kwa  ajili ya ujenzi wa chuo cha MUHAS kampasi ya Kigoma



Mkuu wa mkoa Kigoma Thobias Andengenye akihitimisha hafla hiyo ya utiaji Saini wa ujenzi wa chou hicho alisema kuwa ujenzi huo unatoa uhakikisho wa mkoa kuwa na uhakika wa kukabiliana na wataalam katika sekta ya afya ambapo ujenzi wa chuo hicho chuo hicho na ujenzi wa hospitali ya rufaa ya kanda vitachangia  kufanya miradi hiyo kuwa sehemu ya utalii wa tiba kwa wageni wa ndani na nje ya nchi. 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI