Header Ads Widget

WANANCHI BUGURUNI NJOMBE WAOMBA VIONGOZI WATAKAOKABILIANA NA VIBAKA

 


Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE


Wananchi wa Mtaa wa Buguruni Kata ya Njombe mjini Mkoani Njombe wamelalamikia uwepo wa vibaka ambao wamekuwa tishio katika usalama wao na kuwataka viongozi watakaoshinda katika uchaguzi wa serikali za mitaa kwenda kuweka mkakati wa kupambana nao.



Wananchi hao akiwemo Anna Msigwa na Maneno Ilomo wametoa Kauli Hiyo Katika Mkutano wa Kampeni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wakati Mgombea wa Chama cha mapinduzi CCM na wajumbe wake wakinadi sera zao na kwamba vibaka wamekuwa kikwazo kikubwa kwao.


Akinadi Sera zake kwa wananchi hao Mgombea Uenyekiti Mtaa wa Buguruni Hekima Mhagama amesema suala la Ulinzi na Usalama katika mtaa huo ni kipaumbele cha Kwanza kwake na hivyo atakwenda kukutana na vijana kuweka mkakati wa pamoja wa kukabiliana nalo endapo watamchagua.



Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Njombe Erasto Mpete wakati akizindua Kampeni Hizo amesema serikali ya Chama Cha Mapinduzi imeendelea kutekeleza miradi mingi ya mabilioni ya Fedha na kwamba vyama vya Upinzani vinapaswa kuendelea kuwakumbusha pale wanaposahau kutekeleza.


Aidha Mpete ambaye ni Diwani wa Kata ya Utalingolo amesema katika kipindi cha miaka kadhaa iliyopita Kata ya Njombe mjini Imetekelezwa miradi ya zaidi ya Shilingi bilioni mbili na Hivyo endapo wananchi watawachagua wenyeviti na wajumbe wa CCM Itakuwa rahisi kuendelea kupata fedha nyingine za kutekeleza miradi mingine.



Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Njombe Mjini Alatanga Nyagawa amesema Tayari serikali ya Chama cha Mapinduzi CCM Inaendelea kutekeleza  miradi mbalimbali ya maendeleo katika maeneo mengi na hivyo ili mambo yaendelee vyema ni muhimu kukipa kura chama cha mapinduzi ili kukamilisha kazi.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI