Na Matukio Daima App, Bunda.
Wakulima wa zao la Pamba katika Kijiji cha Hunyari, wilaya ya Bunda Mkoani Mara wameanza kunufaika kwa kulimiwa mashamba yao na Trekta kupitia mpango wa serikali ili kuongeza tija ya Pamba.
Wakulima hao wameanza kufurahia huduma hiyo kupitia Trekta zilizotolewa na serikali kwa kushirikiana na Wanunuzi wa Pamba katika msimu wa Kilimo wa 2024/2025.
Kwa mujibu wa taarifa kwa umma kupitia ukurasa wa Bodi ya Pamba, inaeleza kuwa Mpango wa kulimia wakulima kupitia Trekta ni mojawapo ya Mkakati wa Bodi ya Pamba Tanzania kuweza kuongeza uzalishaji wa Pamba kwa wakulima kufikia Tani 1,000,000 ifikapo msimu wa 2025/2026.
Mkakati huu ulizinduliwa rasmi mwezi Septemba na Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe wilayani Igunga Mkoani Tabora ambapo jumla ya Matrekta 400 yametolewa na serikali nchi nzima ili kuwezesha wakulima wa pamba kuandaa mashamba yao kwa gharama nafuu na Kwa wakati.
Aidha, wilaya ya Bunda imepokea jumla ya Trekta kumi ambazo zimesambazwa kwenye kata za wakulima na zenye uzalishaji Mkubwa wa Pamba.
0 Comments