NA HAMIDA RAMADHAN,MATUKIO DAIMA APp Dodoma
SHEKHE Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mustapha Rajabu Shabaan ametunukiwa tuzo ya heshima ya Udaktari wa Heshima (PhD) kutoka taasisi ya elimu ya juu, ikiwa ni kutambua mchango wake mkubwa katika jamii.
Tukio hilo lilifanyika jijini Dodoma na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali, dini, na wananchi.
Akizungumza baada ya kupokea tuzo hiyo, Shekhe Mkuu Mustapha ameeleza furaha yake na kuelezea kuwa heshima hiyo si yake pekee, bali ni ya watu wote wanaoshirikiana naye katika kazi za kijamii na za kidini.
Aidha shekhe awashukuru wadau wote kwa ushirikiano wao, akisisitiza umuhimu wa mshikamano, maadili, na maendeleo endelevu kwa jamii.
Pia alitumia nafasi hiyo kuwashukuru viongozi, wananchi, na taasisi mbalimbali kwa ushirikiano wao, akisisitiza kuwa heshima hiyo si yake peke yake, bali ni ya wote walioshirikiana naye katika kazi za kijamii na za kidini.
Mhadhiri wa masomo na msimamizi kwa njia ya mtandao Dkt Kharid Salaa anafafanua upatikanaji wa udaktari wa farsafa amebainisha kuwa mchango wa Shekhe Mkuu katika kuhamasisha amani, mshikamano wa kidini, na kusaidia maendeleo ya kijamii ulikuwa na umuhimu wa kipekee.
Aidha, walieleza kuwa anastahili kutambulika kwa juhudi zake za kuimarisha maadili ya kijamii na kujenga jamii yenye mshikamano.
Wananchi wa Dodoma walionyesha furaha yao na kumpongeza Shekhe Mkuu kwa kutambuliwa kwa kazi yake. Tukio hilo lilibainisha umuhimu wa kuthamini viongozi wa dini ambao wamejitolea kwa ajili ya maendeleo ya jamii zao.
Katika hafla hiyo, aliudhuria Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Jabir Shekimweri, alimpongeza Shekhe Mkuu kwa heshima hiyo ya juu ambapo amesema kuwa tuzo hiyo ni uthibitisho wa kazi kubwa aliyoifanya Shekhe Mkuu katika kuimarisha mshikamano wa kidini, maadili, na maendeleo ya jamii mkoani humo na hata nje ya mkoa.
"Shekhe Mkuu amekuwa mfano wa kuigwa kwa kujituma katika kuhamasisha amani, mshikamano wa kijamii, na kuongoza kwa maadili. Tunajivunia kuona kazi zake zinatambuliwa na taasisi za kitaifa na kimataifa ,"
Na kuongeza "Hii si heshima kwake tu, bali pia kwa mkoa wetu wa Dodoma," alisema Shekimweri.
Hafla hiyo iliashiria mshikamano mkubwa kati ya viongozi wa kidini na serikali katika mkoa wa Dodoma, ikiwakumbusha wananchi kuhusu umuhimu wa kuendeleza amani na maendeleo endelevu.
Hata hivyo SHEIKH wa mkoa wa Dodoma sheikh Mustafa Rajab Shaabaan ametunukiwa PhD hiyo kwa udhamini wa Outreach Care International Kwa ushirikiano na chuo kikuu cha Cornerstone International College - USA, Lucent University - UK na HHWB College - USA
0 Comments