Header Ads Widget

UVINZA YAWEKA MKAKATI KUMALIZA MIRADI

Na Fadhili Abdallah,Kigoma

HALMASHAURI ya wilaya Uvinza mkoani Kigoma imesema kuwa imeweka mikakati kuhakikisha miradi tisa iliyopaswa kukamilika mwezi Desemba mwaka huu inakamilika kama ilivyopangwa.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilay Uvinza, Fred Milanzi alisema hayo akitoa taarifa kwa waandishi wa Habari wakati wa kikao cha Kawaida cha baraza la madiwani la halmashauri kwa robo ya Julai hadi Septemba mwaka huu.

Milanzi alisema kuwa sehemu kubwa ya miradi hiyo imeshavuka asilimia 50 ya utekeleji wake hivyo wanaamini kwamba kufikia muda huo miradi hiyo ikiwemo ya elimu na afya itakuwa imekamilika tayari kwa ajili ya  kuanza kutumika mapema mwaka ujao.

Akizungumza wakati akifunga kikao hicho cha Baraza Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya Uvinza, Jackson Mateso alisema kuwa kupitia baraza la madiwani wametoa maagizo na maelekezo kwa watendaji na wataalam kuhakikisha miradi yote inakamilika kulingana na muda uliowekwa wa kukamilisha miradi yote.

Mateso alisema kuwa halmashauri imepata fedhaa nyingi kutoka serikali kuu na mapato ya ndani  kwa ajili ya utekelezaji miradi na kazi kubwa tayari imefanyika ambapo kamati za kudumu zimekuwa zikifanya ziara kukagua miradi na kutoa maagizo ambapo mikakati imewekwa kuhakikisha miradi yote ambayo inapaswa kukamilika kufikia Desemba mwaka huu inakamilika.

Awali akizungumza katika kikao hicho cha Baraza Mkuu wa wilaya Uvinza, Dinnah Mathamani ameitaka halmashauri kusimamia utekelezaji wa miradi kuhakikisha inakamilika kwa wakati ikiwemo miradi ya madarasa ili yaweze kutumika mwezi januari mwakani wakati wanafunzi wapya watakapoanza masomo.




 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI