Header Ads Widget

JESHI LA AKIBA WATAKIWA KUJITOLEA ULINZI WA TAIFA.*

Na Mwandishi wa Matukio Daima App.

Serikali wilayani Bariadi Mkoani Simiyu imewataka vijana kujitoa kwenye Mafunzo ya Ulinzi wa Taifa na mipaka yake kwa sababu ndio Jeshi la Kwanza Tanzania.

Aidha, Wazazi wametakiwa kutowaficha au kuwazuia vijana kujiunga na Mafunzo kwa sababu wakati wa Vita vya Idd Amini, Jeshi hilo lilikuwa mstari wa mbele.

Hayo yamebainishwa leo na Mkuu wa Wilaya hiyo, Simon Simalenga wakati akifunga mafunzo ya Jeshi la Akiba yaliyofanyika kwa muda wa miezi minne tangu mwezi Juni.

Amewataka wakufunzi kufanya mafunzo yaliyobora zaidi ili kutengeneza vijana wazalendo ambao watatumika katika shughuli mbalimbali za kiserikali ikiwemo kuimarisha Ulinzi na usalama katika maeneo yao.

"OCD, Wakurugenzi watumieni hawa vijana kusimamia mitihanj, kwenye fursa za kupata kitu nao wapate sababu kila kata wapo...kwenye Uchaguzi wa serikali za Mitaa watumike hawa" amesema Simalenga.

Mkuu huyo wa wilaya amewataka vijana hao kuwa waaminifu, watiifu, wenye nidhamu na wasiopenda rushwa ili kuonyesha Uzalendo wa kweli.

Ameongeza kuwa kupitia mafunzo waliyopata, hatarajii kuona vijana waliopitia Jeshi la Akiba  wakipokea rushwa na wasio na nidhamu, huku akimwagizwa Mkufunzi kutengeneza kanzi Data inayoonyesha tabia za vijana hao.

Awali Mshauri wa Jeshi la Akiba wilaya ya Bariadi, Meja Ramadhan Mwevi amesema wametoa mafunzo ya kisasa  kwa vijana hao ambao wamefundisha Ulinzi na Usalama, matumizi ya silaha, kupamba na Rushwa, Zimamoto na Uokoaji, Uzalendo na kujitegemea.



 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI