Header Ads Widget

SERIKALI YAAHIDI UTULIVU SIKU YA UPIGAJI KURA SERIKALI ZA MITAA TUNDUMA.

 

Na Moses Ng'wat, Tunduma.

KATIBU Tawala (DAS) wa Wilaya ya Momba, Frank Nkinda, amesema kuwa serikali Wilayani humo imejipanga vilivyo kuhakikisha siku ya uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajia kufanyika Novemba 27 mwaka huu, hali ya usalama, amani na utulivu vinatawala.

Alibainisha hayo, Novemba 2 2024, wakati akitoa salama za serikali alipomwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Momba, Elias Mwandobo, wakati wa kikao cha 

Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Mji Tunduma kilichoketi kwa lengo la kupitia taarifa za utekelezaji kwa robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2024/25.

"Kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya, naomba  nilihakishie Baraza lako nikiwa na  kamati ya KUU (Kamati ya Ulinzi na Usalama) tumejipanga vilivyo kuhakikisha kuwa siku ya uchaguzi  aman na utulivu vinatawa" alibainisha Katibu Tawala huyo.

Aidha, Nkinda alitumia fursa hiyo kuwahimiza Madiwani na watumishi wa Halmashauri hiyo, Viongozi mbalimbali wa kisiasa na madhebu ya dini kuendelea kuhamasisha na kuwapa elimu wananchi waliojiandikisha kwa ajili ya kupiga kura kujitokeza kwa wingi kwenda kupiga kura siku ya Novemba 27 mwaka huu.

Awali Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Tunduma, Mwanaisham Nassor, alivitaka vyama vya siasa katika Halmashauri hiyo kuhakikisha  vinazingatia kanuni za uchaguzi zilizowekwa ili kudumisha hali ya aman na utulivu  katika kipindi chote cha mchakato wa uchaguzi huo.

Mwanaisham amesema dhamira ya serikali ni kuhakikisha kunakuwa na uchaguzi huru na wa haki, huku akatoa rai kwa vyama vya siasa kufanya kampen za kistarab bila kuleta taharuki.

Akifunga kikao hicho, Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Ayoub Mlimba, aliwakumbusha wananchi kushirik zoezi la uchaguzi  kwa utulivu huku wakitambua kuwa baada ya kupiga kura kuna maisha yatapaswa kuendelea.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI