Na Matukio Daima, media
MNEC Salim Abri Asas azindua Kampeni za Uchaguzi wa serikali za mitaa vitongoji na vijiji mkoani Iringa awaomba wananchi kuchagua viongozi Bora kutoka CCM kwani ndicho Chama chenye sera nzuri za kuwaletea maendeleo ,kuwa Novemba 27 wasidanganyike kura Zote CCM.
Alisema kuwa Chama Cha mapinduzi kimeendelea kufanya kazi kubwa ya kuwaletea maendeleo wananchi hivyo ili kazi hiyo nzuri iendelee kuwa nzuri zaidi inahitaji viongozi wazuri wenye Uwezo wa kushirikiana na serikali iliyopo madarakani chini ya CCM kutekeleza ilani ya Uchaguzi ya CCM .
Kwani alisema ilani inayotekelezwa ni ilani ya CCM hivyo anayeweza kusimamia ilani hiyo vizuri ni mwenye ilani yake ambaye anatokana na CCM .
Hivyo ni wajibu wa wananchi kuzingatia zaidi Wagombea wanaotoka CCM Kuwapa kura Zote ili wakawajibike kusimamia Ilani hiyo iwapo watachanganya watu utekelezaji wa ilani utakuwa mgomu kwani hao watakaochanganywa ambao si wanaCCM Watakuwa wakikwamisha utekelezaji wa ilani ya CCM.
Hata hivyo Asas alipongeza kazi kubwa na nzuri iliyofanywa na inayondelea kufanywa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ndani ya nchi hii kuwa ni kazi kubwa inayoheshimisha CCM kwani Kila Kona na nchi hii Kuna miradi mikubwa ya fedha nyingi inayojengwa na mingine imekwisha kamilika ikiwemo miradi ya ujenzi wa Hospital za wilaya,Barabara ,Shule ,maji na miradi mingine mingi ambayo Kila mmoja anaiona .
MNEC Asas alisema wakati wananchi wa kawaida wanafurahia miradi hiyo na utendaji mzuri wa Rais Dkt Samia wapo baadhi ya wapinzani kazi yao kubwa ni kubeza Kila kitu hivyo hao ni kawaida yao na kama hivyo ndivyo wananchi wanapaswa kupuuza kejeri zao na kuchagua viongozi bora kutoka CCM.
MNEC Salim Abri Asas ni mlezi wa CCM mkoa wa Ruvuma hivyo amewataka Wana CCM Mkoa huo kukipatia Chama Cha mapinduzi kura za Kishindo Novemba 27 isiwepo hata kura Moja itakayopotea pia kuwahamasiaha wananchi wa vyama vyote kuchagua viongozi bora kutoka CCM.
0 Comments