Header Ads Widget

MHANDISI KUNDO AKABIDHI MIFUKO 150 YA SARUJI KUKAMILISHA MIRADI YA MAENDELEO

 

Na Matukio Daima App.

MBUNGE wa Jimbo la vi Bariadi Mhandisi Kundo Andrea Mathew, ameendelea na ziara yake ya Kata kwa Kata Tarafa ya Dutwa wilayani Bariadi Mkoani Simiyu, ambapo amekabidhi mifuko ya saruji 150 kwa ajili ya ujenzi wa miradi ya maendeleo katika Jimbo la Bariadi.


Katika ziara hiyo, Mbunge huyo ametoa mifuko 100 ya saruji katika Shule ya Msingi ya Goma, iliyopo Kata ya Ikungulyabashi na mingine 50 kwa ajili ya ujenzi wa Ofisi za CCM kata hiyo.


Amesema saruji hiyo itasaidia kukarabati miundombinu ya shule hiyo na kuboresha mazingira ya kujifunzia kwa wanafunzi na ile ya CCM aitasaidia kuboresha ofisi na kurahisisha shughuli za maendeleo zinazotekelezwa na Chama Cha Mapinduzi.

"Ziara hii ni sehemu ya jitihada za kuimarisha huduma za kijamii na kuboresha miundombinu katika kata zote za Jimbo la Bariadi...Nitaendelea kushirikiana na wananchi na viongozi wa kata zote ili kuhakikisha maendeleo yanaendelea kwa kasi" Amesema Kundo.

Mhandisi Kundo ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maji amewataka wananchi kujitokeza kushiriki Uchaguzi wa serikali za Mitaa utakaofanyika Nov 27, 2024 ili waweze kuunda serikali ngazi ya vijiji na Vitongoji yanakoanzia maendeleo.






Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI