Header Ads Widget

ENG KUNDO APITA KUHAMASISHA UCHAGUZI WA AMANI TARAFA YA NGULYATI

 


NaMatukio Daima App.

MBUNGE wa Jimbo la Bariadi, Mhandisi Kundo Andrea Mathew amepita na kifanya ziara ya kuhamasisha wananchi wa Tarafa ya Ngulyati wilayani Bariadi Mkoani Simiyu, wajitokeze kushiriki kwa amani Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika Nov 27, 2024.

Katika ziara hiyo, Mhandisi Kundo amewahimiza wananchi kushiriki kwa wingi na kwa amani katika uchaguzi huo muhimu ngazi ya vijiji na Vitongoji kwa ajili ya maendeleo ya maeneo yao.


Mbunge huyo ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maji amewahakikishia kuwa uchaguzi huo utafanyika kwa amani na utulivu na kwa kuheshimu taratibu za kisheria.

 "Ni jukumu letu sote kuhakikisha uchaguzi huu na utafanyika kwa amani ili tuweze kuunda serikali ngazi ya chini yanakoanzia endelea na maendeleo ya jamii zetu." Amesema Mhandisi Kundo.

Pamoja na kuhamasisha uchaguzi, Mbunge huyo pia alishiriki Misa Takatifu katika Kanisa Katoliki, kigango cha Ikungulyambesi, ambapo alichangia mifuko 100 ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa kanisa hilo, huku akiahidi kuchangoa mifuko mingine 50 zaidi. 

Vilevile, aliwahidi waumini wa kanisa hilo kuwa atawashonea sare kwaya ya kanisa, ikiwa ni sehemu ya kujenga ushirikiano na kuunga mkono shughuli za kijamii.


Katika hatua nyingine, Mbunge huyo alitoa mifuko 200 ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa sekondari ya Kasoli, kwa lengo la kuboresha Mazingira ya Elimu Jimboni kwake.

Alitumia pia fursa hiyo kufanya kikao na Madiwani pamoja na Wagombea wa nafasi za Uenyekiti wa vijiji kupitia CCM katika Tarafa ya Ngulyati na kujadili masuala mbalimbali na kuwasisitiza kufanya Uchaguzi wa amani katika Vijiji vyote.





Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI