Header Ads Widget

JESHI LA POLISI KAGERA LAPOKEA MAGARI KUIMARISHA USALAMA KUELEKEA UCHAGUZI

 



Na Mariam Kagenda Kagera 

Jeshi la polisi mkoani Kagera limepokea magari matano kwa ajili ya kuimairisha  ulinzi na usalama katika kipindi hiki Cha kuelekea  uchaguzi wa serikali za Mitaa utakaofanyika Novemba 27 mwaka huu siku ya Jumatano.



Kamanda wa Jeshi la polisi mkoa wa Kagera Brasius Chatanda amesema kuwa wanachi wasiwe na wasiwasi katika kipindi hiki badala yake wajitokeze kwa wingi kusikiliza sera za Vyama vyote kwenye kampeini pamoja na kujua ni mgombea Gani watampa dhamana ya kuwaongoza.


Amesema kuwa siku ya kupiga kura Novemba 27 wanachi wasiwe na wasiwasi kwa sababu Jeshi hilo limejipanga vizuri kwani  amani na utulivu ndio kipaumbele Cha kwanza .



"Tulikuwa na changamoto ya vitendea kazi , serikali imeliona Hilo na Jeshi la polisi tumepata  vitendea kazi ,hivi karibuni pia tulipokea magari mawili ,natoa wito kwa wananchi kuhakikisha wanasikiliza kampeini kikamilifu ,na kuchagua kwa amani Jeshi la polisi tuko tayari kulinda amani katika mkoa wa Kagera"


Ametoa wito kwa wananchi kuhakikisha wanawachagua viongozi Bora ambao watakuwa nao bega kwa bega katika maswala ya kuwaletea maendeleo.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI