NA HAMIDA RAMADHAN,MATUKIO DAIMA APP DODOMA
WAHITIMU wa chuo cha Mipango ya Maendeleo viijini Dodoma (IRDP) wametakiwa kujiunga katika vikundi vya ujasiriamali kwa lengo la kupata mikopo ya asilimia kumi inayotolewa na Halmashauri ili waweze kujiendeleza kiuchumi.
Hayo yalisemwa jijini Dodoma wakati wa Mahafali ya 38 ya chuo hicho ambapo jumla ya wanafunzi 5589 wamehitimu katika chuo hicho Cha Mipango
Akiongea kwa niaaba ya Waziri wa Fedha Mwigulu Nchemba Kamishna Idara ya Uendelezaji Sekta ndogo ya Fedha , Dkt.Charles Mwamaja amesema kuwa uchumi wa nchi unaendelea kukua vizuri kwa asilimia 1 katika miaka mitano mfulilizo.
Kamishna Dk,Mwamaja alisema
mambo mazuri yanayoonekana katika Sekta mbalimbali ikiwamo ya elimu ni matokeo ya matunda yanayofanywa na serikali ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Dkt Mwamaja aliongeza kuwa serikali ya Rais Dk.Samia imeendelea kutoa mikopo ya elimu ya juu ya Samia Scholarship.
Awali Mkuu wa Chuo cha Mipango Profesa Hozen Mayaya amesema kuwa serikali imeendelea kutoa huduma za kuwezesha miradi mbalimbali ya miundombinu na uchumi huku akisema kuwapo kwa huduma hizo kumekuwa ni kichocheo cha ukuaji wa uchumi nchini.
Prof.Mayaya alieleza kuwa chuo hicho kimeanzisha kituo cha Ubunifu na ujasiriamali ambacho kinalea bunifu za wanawafunzi wake.
Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi wa chuo hicho Profesa Joseph Kuzilwa alisema kuwa jukumu lao ni kuendelea kusimamia miradi yote kwa kuhakikisha inaendana na thamani ya fedha inayololewa na serikali.
Aidha Prof. Kuzilwa alimpongeza Rais Dk.Samia kwa juhudi zake za kusimamia miradi hasa katika Sekta ya elimu.
0 Comments