Header Ads Widget

DIWANI MPETE AWAELEKEZA WANANCHI NAMNA YA KUWAPIGIA KURA VIONGOZI WA CCM NJOMBE

 


Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE

Wananchi wa Kata ya Utalingolo Halmashauri ya mji wa Njombe mkoani Njombe wamesema Katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika hapo Novemba 27 mwaka huu watakwenda kumpigia kura kiongozi atakayekuwa wazi katika utendaji wake ikiwemo kusoma taarifa za mapato na matumizi kila baada ya miezi mitatu kwa mujibu wa sheria.

Katika Mikutano ya Hadhara ya Kampeni za Uchaguzi huo kwa wakazi wa Nole na Ihalula Katika Kata ya Utalingolo wakazi hao wamesema kumekuwa na Changamoto ya viongozi kutowasomea taarifa ya Mapato na Matumizi kila baada ya miezi mitatu jambo ambalo hawako tayari kuona makosa yakijirudia katika uongozi ujao.


Aidha wamesema wanataka kuona viongozi watakaosikiliza maoni ya wananchi na kuyafanyia kazi badala ya kufanya mambo kwa matakwa yao binafsi ilihali wao ndio waliowapa dhamana ya kuwatumikia.


Stanslaus Nyangadzi ni Mgombea uenyekiti katika Kijiji cha Ihalula kupitia chama cha mapinduzi ambaye anasema endapo wananchi watamchagua katika uchaguzi huo kipaumbele chake cha kwanza ni kwenda kuhakikisha ofisi ya serikali ya kijiji inajengwa pamoja na kushughulikia Changamoto nyingine.



Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Utalingolo Erasto Mpete akiwanadi wagombea hao amesema hakuna sababu ya kupiga kura ya hapana ilihali wako chama kimoja na kwamba itarahisisha upatikanaji wa huduma katika maeneo yao.


Novemba 26  Kampeni za Uchaguzi huo zinahitimishwa tayari kwa zoezi la Uchaguzi wa viongozi wa Serikali za Mitaa Hapo Novemba 27  Nchini kote.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI