Na Fadhili Abdallah,Kigoma
MAKAMU WA Raisi Dk.Philip Mpango amepiga kura nyumbani kwake katika kijiji cha Kasumo wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma kwa ajili ya kuchagua viongozi wa serikali za mitaa huku akitaka wananchi kuchagua kwa kuzingatia viongozi wenye maono ya kuwaletea maendeleo.
Aidha Dk.Mpango Amesema kuwa ni muhimu kwa wananchi kutoa ushirikiano kwa viongozi hao kwa
kujitokeza kuwaunga mkono katika shughuli za maendeleo watakazosimamia.
Amesema viongozi wa serikali za
mitaa ni viongozi wa ngazi ya msingi wanaobeba dhamana ya kuwaongoza wananchi
kupata maendeleo kwa manufaa ya vizazi vya sasa na baadaye
Sambamba na hilo Makamu wa Rais ametoa wito kwa viongozi watakaochaguliwa katika uchaguzi wa serikali za mitaakutumia vema nafasi hizo kuwaletea wananchi maendeleo.
Makamu wa Rais amewapongeza wanakijiji wote wa kijiji cha Kasumo waliojitokeza katika kupiga kura kwenye uchaguzi huo muhimu.
kwa kuwa ni muhimu kwa msingi wa maendeleo
0 Comments