NA WILLIUM PAUL, MOSHI.
CHAMA cha Mapinduzi kimelisimamisha Taifa kwa masaa kadhaa baada ya kuzindua rasmi kampeni za uchaguzi wa serikali za mitaa mikoa yote nchini leo.
Zoezi hilo la uzinduzi wa kampeni hizo limetekelezwa na namna yake na ya kipekee baada ya Wajumbe wa Halmashuri kuu ya Kamati kuu kila mmoja kuzindua kampeni hizo katika mkoa ambao ndio mlezi wake upande wa chama.
Mkoani Kilimanjaro, Katibu wa Nec Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Rabia Hamid alizindua kampeni hizo katika viwanja vya soko la Pasua kata ya Bomambuzi manispaa ya Moshi alisema kuwa, mwaka huu chama hicho kimefanya uzinduzi wa kampeni kwa staili ya aina yake lengo likiwa ni kuwafikia wananchi kwa ukaribu zaidi.
Katibu huyo wa SUKI alisema kuwa, uzinduzi huo ni salama kwa vyama vya upinzani kutambua kuwa chama hicho hakina jambo dogo na kuwataka kutotabiri mbinu wanazokujanazo CCM kwani mwakani katika uchaguzi mkuu watakuja na mbinu nyingine.
"Hii ni salama kwa wapinzani wetu watambue ccm inatambua umuhimu wa kuweka serikali za mitaa madarakani kwani ndio watu muhimu wanaokaa na wananchi na kuwataka kutotabiri kuwa mbinu iliyotumika sasa itatumika tena mwakani" Alisema Rabia.
Alisema kuwa, Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amekuwa halali akihakikisha anapambana kutafuta fedha za kuleta miradi mbalimbali ya maendeleo na kuwataka wananchi kumlipa kwa kuwachagua viongozi wa serikali za mitaa wanaotokana na chama chake CCM ili waungane kwa pamoja kusukuma mbele maendeleo.
Mjumbe huyo wa Nec alisema kuwa, ili kurahisisha kazi ya maendeleo wananchi wanajukumu kubwa la kufanya maamuzi sahihi Novemba 27 mwaka huu kwa kuwachagua wagombea wanaotokana na ccm.
Aidha kiongozi huyo alisema kuwa, wapo watu wanatabia ya kuleta mtafaruko na matabaka miongoni mwa wananchi ndani ya nchi na kuwaomba wananchi kuwapuuza wanasiasa hao ambao hawalitakii mema Taifa.
Pia alidai kuwa, chama hicho kwa sasa kimeandaa tamko ambapo linaonyesha nini kimefanyika katika serikali za mitaa na viongozi hao watakapochaguliwa wataenda kufanya nini kuanzia mwaka 2024 hadi 2029.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi mkoa wa Kilimanjaro, Patrick Boisafi alisema kuwa, chama hicho kimesimamisha wagombea katika vijiji vyote 519, mitaa 60 na vitongoji 2257 za mkoa wa Kilimanjaro.
Boisafi alisema kuwa, kunamahusiano makubwa ya uchaguzi huo wa serikali za mitaa na viongozi waliopo madarakani kwa sasa na kuwaomba wananchi kuwachagua wagombea wanaotoka katika chama kimoja ili kushirikiana kupeleka maendeleo kwao.
Mwisho..
0 Comments