Header Ads Widget

ARUSHA NA SWEDEN ZAKUBALIANA KUENDELEA KUSHIRIKIANA KUKUZA SEKTA YA ELIMU MKOANI ARUSHA.

 


Na Jusline Marco;Arusha


Mkuu wa Mkoa wa Arusha Paul  Makonda amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Sweden nchini Tanzania Mhe. Balozi Charlotta Ozaki Macias, muda mfupi  baada ya kuwasili kwenye ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo leo Novemba 20, 2024.


Katika mazungumzo yao Mhe. Balozi Charlotta amafanya makubalino na Mkuu huyo wa Mkoa ambapo ameahidi kuendeleza mahusiano ya muda mrefu yaliyokuwepo kati ya pande hizo mbili hasa katika kuwanufaisha wananchi wa pande hizo mbili kisekta.



Balozi Charlotta yuko mkoani Arusha akiwa ameambatana na wadau wa Shirika la Kimataifa kutoka Umoja wa Ulaya linalofadhili miradi ya Elimu (GPE) kwa lengo la kukagua utekelezaji na maendeleo ya miradi hiyo,  iliyogharimu zaidi ya Bilioni 4 kwaajili ya kusaidia maendeleo ya sekta ya elimu katila mkoa wa Arusha


Hata hivyo Mkuu wa Mkoa wa Arusha Paul Makonda ameahidi kuhakikisha kuwa miradi hiyo inafanya kazi kama ilivyotarajiwa ya kuhakikisha wanafunzi wanasoma kwenye miundombinu bora na rafiki muda wote ili kurahisisha ufundishaji na kujifunza kwa wanafunzi.


Shirika la Kimataifa kutoka Umoja wa Ulaya linalofadhili miradi ya Elimu (GPE) chini ya Mwenyekiti wa bodi na Rais Mstaafu wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete limetoa ufadhili wa elimu kwa wadau mbalimbali katika kuimarisha mifumo bora ya elimu kwa nchi zaidi ya 89 ikiwemo Tanzania, ambapo huyaweka pamoja mataifa yanayoendelea ili kusaidia katika uboreshaji wa Elimu duniani.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI