Header Ads Widget

WAZIRI WA ELIMU AWATAKA WALIMU KUTOINGIA KWENYE MKUMBO WA WALIOKENGEUKA

 



Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE


Wakati Tanzania ikiungana na mataifa mengine kuadhimisha siku ya Walimu Duniani Waziri wa elimu Sayansi ya Teknolojia Profesa Adolf Mkenda amewataka walimu wasiingie kwenye mkumbo wa wachache wao wanaokengeuka.


Profesa Mkenda ametoa kauli hiyo mkoani Njombe wakati akizungumza na walimu hao na kwamba haiwezekani walimu wakachafuka kupitia walimu wachache na kwamba serikali inaendelea kuwapigania juu ya maslahi yao.


Aidha Waziri Mkenda amesema Serikali imeandaa muongozo maalumu wa kushughulikia stahiki zao yakiwa ni Maelekezo mahsusi ya Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dokta Samia Suluhu Hassan kwani anawathamini sana walimu.



Katibu tawala mkoa wa Njombe Judica Omary Amewataka walimu kuendelea kushikamana kwani Mazingira yao ya kazi yanahitaji zaidi umoja.


Baadhi ya walimu mkoani Njombe akiwemo Innoncent Mwinyibohari Benard William na Neema Nzowa Wamesema kauli ya Waziri wa elimu inawapa molari katika kazi na kwamba wataendelea kushikamana huku wakiomba suala la Kikokotoo kufanyiwa kazi.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI