Na Fadhili Abdallah,Kigoma
MKUU wa wilaya Kigoma Dk.Rashidi ChuaChua amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya Kigoma kuwasimamisha kazi watumishi wanne wa halmashauri hiyo kupisha tuhuma za matumizi mabaya ya madaraka wakiwa na nia ya kufanya ubadhirifu katika mradi wa ujenzi wa hospitali ya wilaya ya Halmashauri hiyo.
Dk.Chuachua alitoa maagizo na maelekezo hayo katika kikao cha majumuishi na watumishi wa halmashauri ya manispaa ya Kigoma baada ya Mkuu huyo wa wilaya Kufanya ukaguzi na kujionea maendeleo ya mradi huo kujiridhisha na tuhuma alizozisikia.
Katika mkutano huo Mkuu huyo wa wilaya ameagiza kusimamishwa kazi kwa Afisa utumishi wa manispaa hiyo, Idrisa Naumanga, Afisa Manunuzi, Anna Magolwa, Afisa TEHAMA, Haji Omari na Mhaandisi wa Manispaa, Eliazari Ndayisaba.
Akitoa hitimisho kuhusiana na hatua hiyo Mkuu huyo wa wilaya alisema kuwa hatua hiyo inalenga kufanyika kwa uchunguzi wa kadhia hiyo baada ya jambo hilo kukabidhiwa kwa Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) akikata pia nyaraka zote za mradi huo zikabidhiwe TAKUKURU.
0 Comments