Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE
Waziri wa elimu Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda amewataka wanafunzi wa Shule mpya ya sekondari Nyombo Mkoani Njombe kutowaangusha wazazi wao kwa kusoma kwa bidii kwa serikali imejenga shule hiyo na kutoa elimu bila malipo.
Profesa Mkenda ametoa kauli hiyo wakati akiweka jiwe la msingi katika shule hiyo ambayo imetajwa kuwa mkombozi kwa watoto wa kata ya Ikuna.
Mwenyekiti wa kijiji cha Nyombo Alfred Kaduma anasema kujengwa kwa shule ya Sekondari Nyombo kumesaidia kupunguza changamoto ya mlundikano wa wanafunzi katika shule Mama ya Sekondari Ikuna.
Mkuu wa shule ya Sekondari Nyombo Anastanzia Mchemwa amesema shule hiyo ilipokea zaidi ya shilingi Milioni 583 na baadhi ya majengo ikiwemo maabara hayajakamilika.
Diwani wa kata ya Ikuna Valentino Hongoli ambaye ni mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Njombe amesema watoto walikuwa wanatembea umbali mrefu mpaka Ikuna sekondari jambo ambalo kujengwa kwa shule hiyo kumesaidia kupunguza adha kwa wanafunzi.
Mbunge wa Jimbo la Lupembe Edwin Swalle amesema Rais Samia amedhamiria kuwakomboa watanzania kwa kuanza na elimu na ndio maana anajenga shule kila pahala
Baadhi ya wanafunzi akiwemo Omben Mwinami Wanakiri kusaidika pakubwa kwa kupunguziwa umbali mrefu wa kutembea huku wakiahidi kusoma kwa bidii na na Mwalimu Ditrick Mbifile kwa niaba ya walimu wenzie akiahidi kuongeza juhudi katika ufundishaji.
0 Comments