Header Ads Widget

WANAWAKE HALMASHAURI YA WILAYA YA KIBAHA WATAKIWA KUJIANDIKISHA KUWANIA NAFASI ZA UONGOZI.

 


WANAWAKE Wilayani Kibaha kujitokeza kujiandikisha kwa wingi kwenye daftari la wapiga kura na kuwania nafasi za uongozi kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba mwaka huu.

Hayo yalisemwa na Makam Mwenyekiti Halmashauri Wilaya ya Kibaha Halima Jongo aliyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari Mlandizi Kibaha na kuwa kwanza wanapaswa kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura ambalo limeanza Oktoba 10 na litadumu kwa siku 10 hadi Oktoba.


Alisema kuwa wanawake wanapaswa kujitokeza kwa wingi kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura ili wapate nafasi ya kupiga kura pia kuweza kuwania nafasiza uongozi ambazo zitakuwa wazi baada ya viongozi waliopo madarakani kumaliza muda wao.


"Nawapa moyo wanawake wenzangu kujitokeza kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura pia wawanie nafasi za uongozi badala ya kuwaachia watu wengine ikiwa nao wanasifa ya kuwa viongozi,"alisema Jongo.


Aidha alisema kuwa waowana uwezo mzuri wa kuongoza hivyo wanapaswa kujiamini wasiwe na hofu na wanapaswa kujiamini wala wasiwahofie wanaume kikubwa nikuingia na kupambana kwani nafasi hizo ziko wazi kwa mtu yoyote na siyo kwa wanaume pekee.


"Baadhi ya wanawake hawajiani kwa sababu ya kuishi maisha ambayo ni mabaya hali

ambayo inasababisha wanapoingia kwenye kinyanganyiro wanakumbana na vikwazo na kusemwa vibaya kutokanana mazingira waliyokuwa wakishi hivyo tabia njema itawafanya wawe huru,"alisema Jongo.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI