Header Ads Widget

WACHIMBAJI MADINI, MC EDWIN LUVANDA WAMPA TUZO RAIS SAMIA

 


Na Thobias Mwanakatwe CHUNYA


WACHIMBAJI wa madini katika mikoa ya Songwe na Mbeya kwa kushirikiana na MC Edwin Luvanda Branding and Entateiment Company wamemtunuku tuzo Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutambua mchango wake katika kukuza sekta ya madini hapa nchini.


Tuzo hiyo waliikabidhi juzi kwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya,Juma Homera, wakati wa hafla ya usiku wa dhahabu iliyofanyika wilayani Chunya na kuwashirikisha wachimbaji madini kutoka mikoa ya kimadini ambayo ni Mbeya,Chunya na Songwe ambayo iliandaliwa.


Mkurugenzi wa kampuni ya MC Edwin Luvanda Branding and Entateiment, Edwin Luvanda, alisema wameamua kutoa tuzo hiyo kwa rais kwani amekuwa mstari wa mbele katika kukuza sekta ya madini ambapo hivi sasa wachimbaji wananufaika madini ukilinganisha na huko nyuma.


Nao Mwenyekiti wa Chama cha Wachimbaji Madini Mkoa wa Mbeya,Njumbo Mtawa na Kaimu Mwenyekiti wa chama cha Wachimbaji madini Mkoa wa Songwe,Goodluck Mungule, walisema Serikali imefanya kazi kubwa kuinua sekta ya madini ambapo hivi sasa kuna soko la uhakikika la kuuza madini hapa nchini.


"Zamani mfano.sisi wachimbaji dhahabu tulikuwa tukilazimika kusafiri kwenda Dar es Salaam au.mkoani kwa ajili ya kwenda kuuza madini hali ambayo ilikuwa hatari kiusalama usumbufu huo hivi sasa haupo masoko yanapatikana karibu," alisema Mtawa.


Naye Mkuu wa Mkoa Mbeya,Homera alisema kwa kutambua kuwa dhahabu ni uchumi,biashara na pia ni maisha atawaelekeza Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wafike kutoa elimu kuhusu kodi mpya ya asilimia 2 wanayotozwa wachimbaji ili wawe na uelewa mzuri.


"Alikuja Kamishna wa TRA mkoani kwetu ambapo alifika hadi kwenye mpaka wa Kasumulu uliopo wilayani Kyela ambapo aliahidi kushughulikia changamoto zote zinazowakabili wachimbaji," alisema.


Homera aliipongeza kampuni ya MC Edwin Luvanda Branding and Entateiment kwa kuandaa maonesho ya vifaa vinavyotumika kwenye uchimbaji pamoja hafla ya usiku wa dhahabu na kwamba mwaka yatafanyika mjini Mbeya.


Aidha, Mkuu huyo wa Mkoa aliwataka wachimbaji wa madini wakipata pesa zinazotokana uchimbaji wazitumie kwani hakuna atakayeishi milele hapa duniani.


"Ukipata pesa kula maisha hakuna atakayeishi hapa duniani milele," alisema Homera na kuwatangazia wachimbaji hao kuwa mkoa umeandaa festiva 2024 ya nyama choma itakayofanyika ufukwe wa Matema ziwa nyasa wilayani Kyela," alisema.




Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI