Header Ads Widget

RC ANDENGENYE ATAHADHARISHA MUDA MCHACHE WA KUJIANDIKISHA ULIOBAKI

 


Na Fadhili Abdallah,Kigoma

 

MKUU wa mkoa Kigoma Thobias Andengenye amejitokeza kujiandikisha kwenye daftari la wakaazi kwa ajili ya uchaguzi wa viongozi wa serikali za mitaa na kusema kuwa watu wengi ambao hawatajiandikisha sasa watapoteza haki yao ya kupiga kura.

 

Andengenye ambaye alijandikisha katika ofisi ya Mtendaji wa kata ya Kigoma Mtaa wa Shede manispaa ya Kigoma Ujiji akieleza kuwa vitambulisho vya kupigia kura vilivyotolewa na Tume Huru ya Taifa ya uchaguzi (INEC) havitatumiki kwenye uchaguzi wa mitaa hivyo amehimiza wananchi wa mkoa Kigoma kutumia vizuri siku chache zilizobaki Kwenda kutimiza haki yao ya kikatiba na kisheria ya kujiandikisha kwani huenda baada ya zoezi hilo kukamilika sasa muda usingezwe kulingana na kalenda ya uchaguzi ilivyo.

 

Pamoja na hilo Mkuu huyo wa mkoa alisema kuwa ni vizuri wananchi kuwa waangalizi  wa uchaguzi huo katika maeneo yao kwa kuwatambua na kuwafichua raia wa nje  ambao hawana sifa ya kuandikishwa na kuwa wapiga kura.

 

Akieleza muitikio wa watu kujitokeza kujiandikisha katika zoezi hilo kwa ajili ya uchaguzi wa serikali za mitaa alisema kuwa zoezi lilianza kwa kusuasua lakini wameoongeza juhudi ambazo wanaamini zitawezesha kufikia lengo la uandikishaji lililowekwa.

 

Mmoja wa wananchi wa manispaa ya Kigoma aliyekutwa akijiandikisha katika kituo cha Metological manispaa ya Kigoma Ujiji alisema kuwa amejitokeza kutimiza haki yake ya kuchagua viongozi na kuhimiza watu wengi Zaidi kujitokeza ili waweze kuchagua viongozi wanaowataka.

 



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI