Header Ads Widget

RAIS DKT SAMIA MGENI RASMI MIAKA 50 YA KANISA LA AICT MAGOMENI

 


Na Fatma Ally Matukio DaimaApp, Dar


Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Misa maalum ya kumtukuza, kumsifu, kumuabudu na kumuomba katika kuelekea kuadhimisha jubilee ya miaka 50 (Golden Jubilee) ya Kanisa la AICT Pastoreti ya Magomeni tangu kuanzishwa na kutoa huduma.


Akizungumza na waandishi wa habari Askofu wa AICT Dayosisi ya Pwani Philipo Magwano Mafuja amesema kuwa shughuli hiyo itafanyika tarehe 27, Octoba 2024, ambapo amewataka mamilioni ya waumini wa kabisa hilo kila mahali nchini Tanzania kujumuika nao.


"Tunafurahi kutumia nafasi hii kuwataarufu mamilioni ya waumini kujumuika nasi katika shughuli hii itakayofanyika hapa Kanisa la AICT Pastoreti ya Magomeni ambayo itakwenda sambamba na na harambee ya kukamilisha ujenzi wa Kanisa unaondelea kanisani hapa "amesema Askofu Mafuja.


Amesema kuwa, kuelekea siku hiyo watakuwa na shughuli mbalimbali za kiroho na Kijamii ikiwemo Tamasha la Uimbaji, Maombi, shughuli za Kijamii na matendo ya huruma na upendo kwa jamii ya watanzania wanaowazunguka na wanaoishi upendo na kushikwa mkono.


"Mfano tunapanga kugawa mitungi ya gesi kuunga mkono juhudi za Mhe Rais Dkt Samia katika ajenda ya nishati safi na kutembelea vituo vya watoto yatima kuwajulia hali na kushirikiana nao, naomba niwalike wote muje tushiriki pamoja katika ibada ya Misa hii"amesema Askofu Mafuja.


Ameongeza kuwa,wakiwa kama washiriki wa mwili wa kristo, wamepata baraka nyingi na hatua muhimu katika safari yao ya miaka 50, pamoja na kufanya tafakuri wameona ni fahari na ibada njema kumrudishia bwana shukurani, heshima, sifa na utukufu Kwa ajili ya walipotoka, walipo na wanapokwenda.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI