Header Ads Widget

VITUO 2,374 KUTUMIKA KUANDIKISHA WAPIGA KURA SERIKALI ZA MITAA PWANI

 


MKOA wa Pwani umeweka jumla ya vituo 2,374 vya kuandikisha wananchi kwenye Daftari la wapiga kura kwa ajili ya uchaguzi wa serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 27 mwaka huu.


Akizungumza baada ya kuzindua zoezi hilo kwenye Mtaa wa Mkoani A uliopo Kata ya Tumbi Wilaya ya Kibaha Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge amesema kuwa idadi hiyo inatokana na sensa iliyofayika ambapo alisema kuwa vijana wengi watakuwa wamefikisha miaka 18 hivyo kuwa na sifa za kujiandikisha kupiga kura.


Kunenge amesema kuwa mkoa una jumla ya Vijiji 417, vitongoji 2,028 na Mitaa 72 ambapo wananchi kwenye maeneo hayo wanapaswa kwenda kujiandikisha ili wapate fursa ya kupiga kura itakapofika wakati wa uchaguzi.


Kwa upande wake mmoja ya watumishi wa Halmashauri ya Mji wa Kibaha ambaye ni moja ya watu waliokwenda kujiandikisha Simon Mwaiteleke amesema kuwa hiyo ni nafasi yake ya kumfanya ili aweze kuja kupiga kura kwa viongozi kwenye mtaa wake.


Naye Saumu Almasi amesema kuwa hiyo ni fursa kwao wananchi kuchagua viopngozi wa Mtaa kuanzia mwenyekiti na wajumbe wake hivyo anaona ni fursa ya kumchagua kiongozi ambaye ana sifa ya kuongoza mtaa anaotoka.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI