Header Ads Widget

"TUNAKAMILISHA MABORESHO MAKUBWA BANDARI YA KIGOMA "-TPA

 



Na Fadhili Abdallah,Kigoma

 

MAMLAKA ya usimamizi wa bandari (TPA) imesema kuwa maboresho makubwa yanayofanywa katika bandari za Ziwa Tanganyika ikiwemo bandari ya Kigoma yanalenga kukidhi mahiti ya wateja wanaotaka kusafirisha shehena kubwa ya bidhaa Kutoka Tanzania kwenda  nchi za ukanda wa maziwa makuu.

 

Meneja wa bandari za ziwa Tanganyika, Edward Mabula alisema hayo akifunga wiki ya huduma kwa wateja ambapo mamlaka hiyo ofisi ya Kigoma iliandaa chakula cha jioni kwa wateja wake ambapo alisema kuwa tangu mwaka 2018 uboreshaji ulianza katika bandari za ziwa Tanganyika ambapo kiasi cha shilingi bilioni 108 kilianza kutumika ikiwa ni sehemu ya mpango wa TPA katika kuboresha bandari za ziwa Tanganyika.

 


Sambamba na hilo alisema kuwa mwaka jana Shirika la maendeleo la Japan (JICA) lilitenga kiasi cha shilingi  Bilioni mbili kwa ajili ya kuboresha bandari ya Kigoma mpango ulioanza mwaka jana na serikali kupitia (TPA) imeongeza fedha Zaidi ambapo mpango huo utakamilika mwakani.

 

Baadhi ya wateja waliohudhuria hafla hiyo wanaotoa huduma katika bandari ya Kigoma akiwemo Mbaraka Amour Saidi Mkurugenzi wa Falcon Marine ambao ni wakala wa meli katika ziwa Tanganyika alisema kuwa maboresho makubwa yanayotakiwa kufanya kwa sasa ni kuboresha zana za kupakia na kupakua shehena kwani winchi zilizopo hazizidi tani 60 wakati ipo mizigo ya tani Zaidi ya 100 inayopaswa kushughulikiwa kupitia katika bandari hiyo.

 


Naye Mkurugenzi wa kampuni ya shegema ambao ni  Wakala wa Huduma za meli katika bandari ya Kigoma, JULIANA MUTABIIRWA alisema kuwa kazi zinafanyika vizuri tatizo ni vifaa vya kushushia na kupandisha shehena bado yanahitajika maboresho kutokana na mizigo mizito kupitishwa bandari hapo ambayo winchi zilizopo bandari hapo zinazidiwa uwezo.

 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI