Viongozi wa Serikali za mitaa wakiwemo wenyeviti wa mitaa, vitongoji , wajumbe wa Serikali za vijiji wanaomaliza muda wao wa uongozi , Manispaa ya Lindi Mkoani Humo wametakiwa kuwahamasisha vijana kushiriki kugombea nafasi mbalimbali Katika uchaguzi wa Serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika November 27, 2024
Wito huo umetolewa Leo oktoba 05/2024 na Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini wa Manispaa ya Lindi Bi.Hajra Hashim wakati wa ghafla fupi ya kuwaaga viongozi wa Serikali za mitaa wa kata ya chikonji huko manispaa ya Lindi
Bi Hajra Amesema kupitia wao wanayonafasi ya kuzungumza na vijana Umuhimu wa kugombea na kushika nafasi za uongozi ikiwa ni mwanzo mzuri wa kujiimarisha kisiasa wakiwa bado vijana pamoja na kuwa chachu ya Maendeleo katika Maeneo yao
Moses Mkoveke ni Afisa Maendeleo ya Jamii halmashauri ya Manispaa ya Lindi akatumia fursa hiyo pia kueleza Umuhimu wa wanawake kushiriki na kugombea nafasi mbalimbali za uongozi
Amesema Serikali inaimiza na kuwakumbusha wanawake kuendelea kugombea Katika nafasi mbalimbali za uongozi ili wawe chachu ya kutetea maslahi yao
" Akina mama mmekuwa mstari wa nyuma na sasa Serikali inawahimiza na kuwakumbusheni kwamba mjitahidi na mjitokeze na imeanza kutenga fulsa zenu kwa usawa kama mnavyofahamu hivi sasa mikopo ya asilimia 10 imerudi na hela zenu pale zipo asilimia 40 sasa ili muweze kuzisimamia vizuri ni lazima muwe pia kwenye sehemu ya uongozi" .
Esha salaam Mtandi ni Mtendaji wa Kata ya chikonji alitumia fursa hiyo kuwakumbusha viongozi wa Serikali za mitaa wa kata hiyo wanaomaliza muda wao kuendelea kuwa waaminifu na waadilifu Katika kutunza Siri za Serikali
0 Comments