Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE
Serikali imeahidi kupeleka vifaa tiba vya afya vyote katika kituo kipya cha Afya Ikondo wilayani Njombe mkoani Njombe ili wananchi waanze kupata huduma.
Akiweka jiwe la msingi katika kituo hicho Waziri wa elimu Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda amesema baada ya kupelekwa kwa vifaa tiba itasaidia wananchi kupata huduma bora zikiwemo za upasuaji ambazo zimekuwa changamoto kubwa nchini.
Mbunge wa Jimbo la Lupembe Mhe.Edwin Swalle amesema tayari serikali imeshapeleka baadhi ya vifaa tiba kwa ajili ya huduma za Afya katika kituo hicho ambacho kipo mwishoni kukamilika.
Mganga mfawidhi wa kituo cha Afya Ikondo Dokta Charles Kehogo amesema Jumla ya shilingi Milioni 610 zimepokelewa na kujenga kituo hicho na zimesalia milioni 10 kwa ajili ya jengo la Mama na mtoto.
Aidha Dokta Kehogo amesema kungali na baadhi ya changamoto zilizopo katika eneo hilo ikowemo kukosekana kwa mtandao wa simu wa uhakika kwa ajili ya mawasiliano,kukosekana kwa gari la wagonjwa kwani kituo hicho kimeanza kutoa huduma.
0 Comments