Na Hamida Ramadhan, Matukio Daily App Dodoma
UMOJA wa wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT) wamelaani vilali kitendo cha wanawake wa chama cha Demokrasia na Maendeleo ( BAWACHA) kuchoma kitenge chenye picha ya Rais samia suluhu Hassan kwa madai kuwa ameshindwa kukamilisha mambo Malimbali ikiwemo kukithili kwa ugumu wa maisha.
Hatua hiyo imekuja baada ya wanawake Hao (BAwacha) kuchoma vitege walivyogawiwa na UWT kama sare kwenye kongamano la siku ya wanawake duniani machi 8 ,2023 jambo linalotazamwa na UWT kuwa ni kuishiwa sera.
Hayo yamesemwa leo jijini hapa na Mwenyekiti wa UWT Taifa Marry Chatanda alipokuwa akiongea na waandishi wa habari jijini hapa ambapo ameeleza kuwa tukio hilo ni lakitoto ,upuuzi huku akiwataka (BAWACHA) kuibua sera zenye mashiko kwa jamiii.
" Kwanza niseme jambo kitenge kilichochomwa ni kitenge kinachoashiria kishindo cha utekelezaji wa ilani ya chama cha Mapinduzi CCM 2020/2025, kitenge hicho kilitengenezwa na UWT Taifa ikiwa ni sare kwa ajili ya kongamano la kumpongeza Rais samia kwa kazi nzuri alitoifanya kwa kipindi cha miaka miwili iliyofanyika machi 19 2023 , "amesema na kuongeza ;
Toleo la kwanza la kitenge hicho lilitolewa machi 13 2023 hivyo ni uongo kusema kuwa Rais Samia ndio aliyewagawia vitenge hivyo kwani siku wanafanya baraza lao kitenge kilikuwa bado hakijatengenezwa bali wanachama wa BAWACHA walinunua kitenge hicho ikiwa ni sare kwaajili ya kongamano kwaajili ya kumpongeza Rais samia na tuliwaalika na waliudhuria kwa wingi, "amefafanua
Pamoja na hayo Mwenyekiti huyo pia ameeleza kuwa, "Hivyo kitendo cha wana BAWACHA kununua na kuudhuria kwa wingi kwenye kongamano letu kunaashiria kwamba Rais samia ametekeleza mengi na waliyoyaeleza kwenye baraza kuu la BAWACHA) Machi 8 2023 na kwamba wasiishie kuchoma vitenge bali pia waeleze ukweli waliwezaji kufanya baraza hilo, "amesema Chatanda
Aidha amesema Rais samia amefanya mambo makubwa na mazuri kwa Taifa katika nyanja zote hivyo badala ya kuchoma kitenge ni vyema wakatumia muda huo kutangaza fursa zote za kiuchumi ambazo Rais amekuwa akizipigania.
Katika hatua nyingine Chatanda ameipongeza mahakama ya Dodoma chini ya kituo jumuishi cha utoaji haki kwa kutenda haki kwenye kesi ya kubaka na kumuingilia kinyume cha maumbile binti wa yombo Dovya.
Amesema, "Jana washtakiwa walihukumiwa kifungo cha maisha jela na faini ya milioni moja kila mmoja, huu ni ushindi mkubwa dhidi ya mapambano ya unyanyasaji wa kijinsia, " ameeleza
Aidha amesema UWT inaendelea kutoa wito kwa jamii kuhakikisha inaendelea kulinda haki na kupinga vitendo vyote vinavyoendelea kwenye jamii ili kuwa na usalama na haki.
0 Comments