Na Fadhili Abdallah,Kigoma
Klabu ya mashujaa ya mkoani Kigoma imesema kuwa mipango yake ya kuifanya timu hiyo kumaliza nafasi ya nne kwenye ligi kuu Tanzania Bara imeanza kutekelezwa kwa vitendo.
Mshambuali wa timu hiyo Chrispin Ngushi ametoa Kauli hiyo katika mkutano wa pamoja wa waandishi wa habari na timu hiyo (Mashujaa Media Day) uliofanyika kwenye uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma.
Ngushi alisema kuwa Mashujaa ya msimu huu ina malengo makubwa ya kufanya vizuri kucheza mashindano ya kimataifa mwakani kutokana na usajili mkubwa wa wachezaji uliofanywa na timu hiyo.
Kwa upande wake Nahodha wa timu ya Mashujaa, Masome Mashauri alisema kuwa usajili uliofanywa na timu hiyo mwaka huu, matunzo wanayopata kutoka kwa uongozi na kuungwa mkono na mashabiki imekuwa silaha kubwa ya kuwapa morali wachezaji kuhakikisha wanapambana kila mechi kupata ushindi.
Kocha wa timu ya Mashujaa Mohamed Barres akizungumza katika mahojiano hayo alisema kuwa msimu huu wana timu nzuri na wachezaji wana Morali kubwa hivyo kila mechi kwao wanaichukulia kama fainali ili kupata ushindi akabainisha kuwa mipango ya timu hiyo kwa sasa ni kuhakikisha inamaliza katika nafasi nne za juu.
0 Comments